DKT. GHARIB BILAL AHUDHURIA MKUTANO WA 12 WA NCHI ZA AFRIKA ABUJA,NIGERIA. - Wazalendo 25 Blog

Glory to Story.

Habari Mpya

PRINTING / GRAPHICS / DESIGN : 0784 643 633


PRINTING / GRAPHICS / DESIGN : 0676 643 633

Tuesday 16 July 2013

DKT. GHARIB BILAL AHUDHURIA MKUTANO WA 12 WA NCHI ZA AFRIKA ABUJA,NIGERIA.

 Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akisalimiana na Mfalme Mswati (ii) wakati walipokutana kwenye Mkutano wa 12 wa Afrika unaojadili magonjwa ya Ukimwi, Kifua Kikuu na Malaria (Abuja +12) uliofunguliwa na Rais wa Nigeria Dkt. Goodluck Jonathan, ulioanza mjini Abuja Nigeria na kuhudhuriwa na Viongozi mbalimbali wa Nchi za Afrika. Katikati yao ni Naibu Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa, Mahadhi Juma Mahadhi (kulia) ni Naibu Waziri wa Afya, Dkt. Seif Rashid.
 Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akiwa na baadhi ya Viongozi wenzake wakati wa ufunguzi rasmi wa Mkutano wa 12 wa Afrika unaojadili magonjwa ya Ukimwi, Kifua Kikuu na Malaria (Abuja +12) uliofunguliwa na Rais wa Nigeria Dkt. Goodluck Jonathan,mjini Abuja Nigeria na kuhudhuriwa na Viongozi mbalimbali wa Nchi za Afrika.
 Makamu wa Rais, Dkt. Bilal, Naibu Waziri wa Afya, Dkt. Seif Rashid (kulia) na Naibu Waziri wa Mambo ya Nje, Mahadhi Juma Mahadhi, wakisimama wakati zikipigwa nyimbo za Taifa ukumbini humo.
 Rais wa Nigeria, Goodluck Jonathan (kulia) akiongozana na baadhi ya marais, wakati akiwasili ukumbini hapo kufungua rasmi mkutano huo.
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akishiriki katika Mkutano wa 12 wa Afrika unaojadili magonjwa ya Ukimwi, Kifua Kikuu na Malaria (Abuja +12) uliofunguliwa na Rais wa Nigeria Dkt. Goodluck Jonathan, ulioanza mjini Abuja Nigeria na kuhudhuriwa na Viongozi mbalimbali wa Nchi za Afrika.Picha na Sufiani Mafoto Blog

No comments:

Post a Comment