Matukio :Dk. Gharib Bilal Afungua Mkutano wa Mabunge wa Kujadili Sera za Misitu Afrika. - Wazalendo 25 Blog

Habari Mpya

Glory to Story.


Post Top Ad


10 Jul 2013

Matukio :Dk. Gharib Bilal Afungua Mkutano wa Mabunge wa Kujadili Sera za Misitu Afrika.



 Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akisalimiana na Mkurugenzi wa Baraza la Dunia ya baadaye wa Dunia, 'World Future Council' Alexandra Wandel, wakati alipowasili kwenye Hoteli ya Hyatt Kilimanjaro jijini Dar es Salaam, jana jioni Julai 9, 2013 kwa ajili ya kufungua Mkutano wa Mabunge wa kujadili Sera za Misitu Barani Afrika, uliohudhuriwa na wabunge mbalimbali kutoka Bara la Afrika. Katikati ni Mbunge wa Bunge la Afrika Mashariki, Getrude Mongela.
 Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akihutubia wakati akifungua rasmi Mkutano wa Mabunge wa kujadili Sera za Misitu Barani AFrika, uliofanyika jana jioni kwenye Hoteli ya Hyatt Kilimanjaro, jijini Dar es Salaam.
 Mkurugenzi wa Baraza la Dunia ya baadaye wa Dunia, 'World Future Council' Alexandra Wandel,akizungumza wakati wa ufunguzi wa mkutano huo.
 Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, (katikati) akiwa na Naibu Waziri wa Maliasili na Utalii, Lazaro Nyalandu, (wa pili kulia) Mkurugenzi wa Baraza la Dunia ya baadaye wa Dunia, 'World Future Council' Alexandra Wandel (wa pili kushoto) na Mbunge wa Bunge la Afrika Mashariki, Getrude Mongela (kulia) wakifuatilia moja ya mada zilizokuwa zikitolewa ukumbini hapo kupitia Screen kwa njia ya TV.
Baadhi ya Wabunge wakiwa katika chumba cha mkutano huo, kutoka (kushoto) ni Mbunge wa Kahama James Lembeli, Mbunge wa Mafia, Abdulkarim Shah, Mbunge wa Iringa Mjini, Mchungaji Peter Msigwa na Mbunge wa Kigoma Kusini, David Kafulila, wakiwa katika mkutano huo jana. Kwa picha zaidi bofya hapa>>>

No comments:

Post a Comment

Post Top Ad