CHAMA CHA MAPINDUZI (CCM) NA SERIKALI YA CHINA KUSHIRIKIANA KUJENGA CHUO CHA IHEMI MJINI IRINGA. - Wazalendo 25 Blog

Glory to Story.

Habari Mpya

PRINTING / GRAPHICS / DESIGN : 0784 643 633


PRINTING / GRAPHICS / DESIGN : 0676 643 633

Wednesday 24 July 2013

CHAMA CHA MAPINDUZI (CCM) NA SERIKALI YA CHINA KUSHIRIKIANA KUJENGA CHUO CHA IHEMI MJINI IRINGA.

Kamanda  wa UVCCM mkoa wa Iringa  Salim Abri  Asas kushoto akiangana na katibu mkuu  wa CCM Taifa  Abdulrahman Kinana  leo katika  uwanja  wa ndege Nduli  baada ya  kukamilisha  ziara ya balozi wa china  nchini Bw Lu Youqing  kwa  ajili ya kuanza ushirikiano na CCM kwenye ujenzi wa chuo cha Ihemi

Kamanda  wa UVCCM mkoa  wa Iringa Salima Abri  Asas kulia akiwa na  katibu wa itikadi na uenezi  wa CCM Taifa  Nape Nnauye na mkuu  wa  wilaya ya Kilolo Gerald Guninita  leo katika  uwanja  wa ndege Nduli  
SERIKALI  ya  nchi  ya  China  imekusudia  kushirikiana na chama  cha mapinduzi (CCM)  katika   kufufua  chuo  cha  vijana  Ihemi katika wilaya ya  Iringa  mkoani  Iringa kwa  ajili  ya  kukiwezesha  chuo hicho  kutoa mafunzo ya uongozi kwa  vijana  kutoka  nchi  za Sadac pamoja na nchi ya  China .
Katika kuonyesha mikakati ya  awali ya kuanza  kukifufua  chuo  hicho  balozi   wa  chini  nchini  Tanzania Bw Lu Youqing  leo  amekitembelea  chuo  hicho  chenye eneo la   ukubwa  wa  hekari 1900 na  kuonyesha  kuvutiwa  zaidi na eneo  hilo.
Akielezea  mkakati  huo katibu  wa itikadi na  uenezi  wa CCM Taifa  Nape Nnauye  alisema  kuwa CCM inaompango  wa  kukiendeleza  chuo hicho  kwa  kushirikiano na  serikali ya  China .
“Leo  tumekuja  na  balozi  wa China  kwa  ajili ya  kupaendeleza zaidi ikiwa ni pamoja na  kutoa  elimu ya  uongozi pamoja na  masuala ya  ujasiriamali ambayo yatawafanya  zaidi  vijana  kuweza  kujiajiri  zaidi”
Alisema  kuwa  mpango  wa  kukifufua  chuo  hicho  unataraji kuanza mara  moja  na kuwa hayo ni maamuzi ya  mkutano  mkuu  wa Taifa  ambayo  utekelezaji  wake  unaanza mara  moja .

Nnauye  alisema  kuwa  kutokana  na maamuzi hayo ya mkutano  mkuu  wao  wameanza  kufanyia kazi  suala  hilo kwa  kuwatafuta  wahisani hao  kutoka China ambao  watasaidia  kufanikisha  ujenzi huo ambao  kukamilika  kwake  ni ukombozi mkubwa kwa  vijana nchini nan chi  nyingine .
 
Pia  alisema  kuwa  kuyumba  kwa  chuo  hicho  kunatokana na  mfumo  wa vyama  vingi na kuwa kabla ya  mfumo  wa  vyama  vingi kuanza  chuo  hicho  cha  Ihemi kilikuwa  kikifanya kazi  vema  japo  alisema  kwa  sasa mkakati ni  kukifufua  na kuwa chuo  hicho  kitakamilika  ndani ya mwaka huu .

Kuhusu aina ya mafunzo yatakayotolewa alisema  kwa  sasa ni mapema sana   ila  mara  baada ya  ujenzi  kukamilika  basi aina ya mafunzo yatakayotolewa yatajulikana .

Nnauye  alipoulizwa kuhusu  gharama ya  jumla  itakayotumika  kujenga  chuo  hicho  alisema  kuwa kwa  sasa bado ni mapema kujua  ni kiasi gani kitatumika katika ujenzi na  kuwa hatua iliyopo sasa ni ya awali  zaidi .

Katika  ziara  hiyo ya  balozi  wa China nchini aliongozana na msaidizi  wake Bi.Wang Fang pamoja na katibu mkuu wa CCM Taifa Abdulrahman  Kinana ,katibu  mkuu  wa UVCCM Taifa  Martine Shegela  pamoja na  viongozi mbali mbali  wa chama  na  serikali wilaya na  mkoa  wa Iringa . Kwa habari zaidi usisite kubofya hapa >>>

No comments:

Post a Comment