Afisa
wa Kitengo cha Usalama wa Kampuni ya Mantra Tanzania inayoshughulika na
Mradi wa Uchimbaji Madini aina ya Uranium,uliopo kwenye Kijiji
Mkuju,Wilayani Namtumbo Mkoani Ruvuma, Fredrick Kriel akitoa mada ya
maswala ya Usalama Mgodini wakati wa Semina fupi kwa Baadhi ya
Wanahabari waliofanikiwa kutembelea Mradi huo uliopo pembezoni mwa
Hifadhi ya Taifa ya Seluu na kufahamu mambo mbali mbali juu ya Madini
hayo ya Uraniuam.
Afisa
wa Kitengo cha Usalama wa Kampuni ya Mantra Tanzania,Fredrick Kriel
akionyesha moja ya mambo muhimu na yanayotakiwa kuzingatiwa kwa mtu
yeyote awapo Mgodini.
Meneja
Mkuu wa Maswala ya Usalama, Afya, Mazingira na Ubora wa Kampuni ya
Mantra Tanzania,Cornelis Van Den Berg akifafanua jambo kuhusu mradi huo
wa Madini ya aina ya Uranium wakati wa semina fupi na baadhi ya
Wanahabari walioweza kutembelea Mgodi huo leo,na kuweza kujionea na
kufahamu mambo mbali mbali juu ya Mgodi huo.
Mkuu
wa Kitengo ya Mahusiano wa Kampuni ya Mantra Tanzani,Khadija Pallangyo
akielezea namna Kampuni yake inavyoweza kutoa kipaumbele katika kusaidia
jamii inayouzunguka mradi huko.
Baadhi
ya Wanahabari kutoka vyombo mbali mbali vya habari hapa nchini
wakifatilia mada zilizokuwa zikiwasilishwa na wahusika wa Mradi
huo.Kulia ni Mkurugenzi wa Kampuni ya Montage,Teddy Mapunda ambaye
ameambatana na wanahabari hao,na wa pili kulia ni Mkuu wa Kitengo ya
Mahusiano wa Kampuni ya Mantra Tanzani,Khadija Pallangyo.
Sehemu ya Mandhali ya Mahema ya maofisi ya Kampuni hiyo wakati huu wa Utafiti wa Madini ya aina ya Uranium.
Wanahabari hao wakiwa katika Picha ya Pamoja na baadhi ya viongozi wasimamizi wa Mradi huo.
Afisa
wa Kitengo cha Usalama wa Kampuni ya Mantra Tanzania,Fredrick Kriel
akitoa maelezo ya namna mambo yanavyokuwa pindi wawapo kazini.Kulia ni
Mkurugenzi wa Kampuni ya Montage,Teddy Mapunda na kushoto ni
Mwanalibeneke Othman Michuzi wakisikiliza kwa umakini.
No comments:
Post a Comment