Rais
Jakaya Mrisho Kikwete na ujumbe wake wakitembezwa kwenye makao makuu ya
Mamlaka ya Ustawishaji Upya wa Miji Upya ya Singapore leo Juni 6, 2013
ambapo wanajionea mfano wa jiji hilo ukiwa umetengenezwa mahususi kwa
kuhakikisha mji unapangwa na kusimamiwa kisayansi kwa mipango miji ya
muda mfupi na muda mrefu.
Rais
Jakaya Mrisho Kikwete na ujumbe wake wakitembelea Taasisi ya Elimu ya
ufundi (Institute of Technical education) iliyo sawa na VETA kwa
Tanzania leo Juni 6, 2013.ambapo pamoja na mambo mengine walijionea
jinsi wanafunzi wake wanavyofundishwa kuunda vipuli vya aina mbalimbali
ikiwa ni pamoja na vya ndege.
Rais
Jakaya Mrisho Kikwete na ujumbe wake wakitembezwa kwenye makao makuu ya
Mamlaka ya Ustawishaji mijini ya Singapore .ambapo
wanajionea mfano wa jiji hilo ukiwa umetengenezwa mahususi kwa
kuhakikisha mji unapangwa na kusimamiwa kisayansi kwa mipango miji ya
muda mfupi na muda mrefu.
Baadhi
ya wafanyabiashara walioongozana na Rais Jakaya Kikwete katika ziara ya
kikazi nchini Singapore wakiwa katika picha ya kumbukumbu na mawaziri
walio katika msafara huo. Wa pili kushoto ni Waziri wa
Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa Mhe Bernard Membe akifuatiwa
na Waziri wa Viwanda na Biashara Dkt Abdallah Kigoda na Waziri wa
Uchukuzi Dkt Harrison Mwakyembe (wa tatu) kulia.
Rais
Jakaya Mrisho Kikwete na ujumbe wake katika picha ya pamoja na viongozi
wa Mamlaka ya Ustawishaji Upya ya Miji ya Singapore.
Rais
Jakaya Mrisho Kikwete na ujumbe wake katika picha ya pamoja na viongozi
wa Taasisi ya Elimu ya Ufundi ya Singapore baada ya kutembelea kampasi
yao jijini Singapore Juni 6, 2013.PICHA NA IKULU
No comments:
Post a Comment