

Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akisoma hotuba yake wakati wa Harambee ya Mfuko wa Udhamini wa Elimu ya Juu wa Mwalimu Nyerere, iliyofanyika jana Aprili 8, 2013 katika Ukumbi wa Benki Kuu (BOT) jijini Dar es Salaam. Katika Harambee hiyo zilikusanywa fedha taslimu shilingi milioni 71 na ahadi ya fedha za Kitanzania shilingi milioni 658.

Baadhi ya wadau wa Elimu na wachangiaji wa Mfuko huo, wakimsikiliza Mhe. Makamu wa Rais Dkt. Bilal.

Baadhi ya wadau wa Elimu na wachangiaji wa Mfuko huo, wakimsikiliza Mhe. Makamu wa Rais Dkt. Bilal.

Baadhi ya wadau wa Elimu na wachangiaji wa Mfuko huo, wakimsikiliza Mhe. Makamu wa Rais Dkt. Bilal. Zaidi Bofya HAPA chini

Makamu wa Rais Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akionyesha moja ya Sarafu iliyopigwa mnada katika harambee ya Mfuko wa Udhamini wa Elimu ya Juu wa Mwalimu Nyerere, iliyofanyika katika Ukumbi wa Benki Kuu (BOT) jijini Dar es Salaam, ambayo ilinunuliwa na Mwenyekiti wa Makampuni ya IPP, Reginard Mengi kwa Sh. milioni 20. Kushoto ni Waziri wa Fedha Dkt. William Mgimwa.
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akimpongeza Mwenyekiti wa Makampuni ya IPP, Reginard Mengi, baada ya kununua sarafu kwa Sh. milioni 20, wakati wa Harambee ya Mfuko wa Udhamini wa Elimu ya Juu wa Mwalimu Nyerere, iliyofanyika katika Ukumbi wa Benki Kuu (BOT) jijini Dar es Salaam.

Makamu wa Rais Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akimkabidhi sarafu Dkt. Charles Kimei, baada ya kuinunua sarafu hiyo kwa Sh. milioni 19 katika mnada wa Harambee ya Mfuko wa Udhamini wa Elimu ya Juu wa Mwalimu Nyerere, iliyofanyika katika Ukumbi wa Benki Kuu (BOT) jijini Dar es Salaam.
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akimpongeza Mkuu wa Masoko na Ushirikiano wa Benki ya Stanbic, Abdallah Singano, baada ya kuchangia mfuko huo kiasi cha Sh. Milionio 10 za kizatanzania katika harambee hiyo.
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akimkabidhi zawadi Mwenyekiti wa Makampuni ya IPP, Reginard Mengi, baada ya kununua sarafu kwa Sh. milioni 20, wakati wa Harambee ya Mfuko wa Udhamini wa Elimu ya Juu wa Mwalimu Nyerere, iliyofanyika katika Ukumbi wa Benki Kuu (BOT) jijini Dar es Salaam. Kwa picha zaidi bofya hapa >>>
No comments:
Post a Comment