SAFARI YA MWISHO YA BI. FATMA BINTI BARAKA "BI. KIDUDE". RAIS WA ZANZIBAR DR. ALI MOHAMED SHEIN AHUDHURIA - Wazalendo 25 Blog

Habari Mpya

Glory to Story.


Post Top Ad


18 Apr 2013

SAFARI YA MWISHO YA BI. FATMA BINTI BARAKA "BI. KIDUDE". RAIS WA ZANZIBAR DR. ALI MOHAMED SHEIN AHUDHURIA


 Waumini wa dini ya Kiislamu wakibeba Jeneza lenye mwili wa Marehemu Fatma Baraka 'Bi Kidude', wakati wakiingiza jeneza hilo Msikiti wa Mwembeshauri, kwa ajili ya kuswaliwa kabla ya kuelekea kijijini kwa marehemu, Kitumba Wilaya ya Kati kwa maziko, mchana huu.
  Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, Rais wa Zanzibar, Dkt. Mohammed Ali Mohamed Shein, wakishiriki katika dua maalum ya kumswalia marehemu Fatma Baraka 'Bi Kidude', iliyofanyika mchana huu katika Msikiti wa Mwembeshauri mjini Zanzibar. Bi Kidude anatarajia kuzikwa mchana huu kijijini kwao Kitumba Wilaya ya Kati, Unguja.
Msanii wa muziki wa kizazi kipya Ramadhan Nasib 'Diamond Plutnum' (kulia), akiwa ni mmoja kati ya wasanii waliohudhuria katika dua maalum ya kumswalia marehemu Fatma Baraka 'Bi Kidude', iliyofanyika mchana huu katika Msikiti wa Mwembeshauri, mjini Zanzibar. Bi Kidude anatarajia kuzikwa mchana huu kijijini kwao  Kitumba Wilaya ya Kati, Unguja.

No comments:

Post a Comment

Post Top Ad