MTOTO WA MAREHEMU MORINGE SOKOINE NA MBUNGE WA VITI MAALUM BI. NAMELOK AKIZUNGUMZA KATIKA MASHINDANO YA KUMUENZI BABA YAKE - Wazalendo 25 Blog

Glory to Story.

Habari Mpya

PRINTING / GRAPHICS / DESIGN : 0784 643 633

Saturday, 13 April 2013

MTOTO WA MAREHEMU MORINGE SOKOINE NA MBUNGE WA VITI MAALUM BI. NAMELOK AKIZUNGUMZA KATIKA MASHINDANO YA KUMUENZI BABA YAKE


Mh. Namelok Moringe Sokoine akikabidhiwa  cheti cha kushiriki mbio za Edward Moringe Sokoine Mini Marathon na mkuu wa mkoa wa Arusha mh. Magesa Mlongo jana wilayani Monduli Arusha.

Namelok Sokoine ni binti wa hayati Moringe Sokoine ambaye ni mfano wa kuigwa na wanawake wote nchini kwa kusimama kidete katika maandalizi ya kumbu kumbu za baba yake, aliyefariki mnamo tarehe 12/4/1984 kwa ajali ya gari wakati huo akiwa ndiye Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano Wa Tanzania.


Dada huyu ni mchapa kazi, anapenda watu wote bila kujali cheo au kitu chochote alichonacho. Namelok Sokoine amewashukuru viongozi na watu wote waliohudhulia siku ya kumbu kumbu ya hayati waziri mkuu Edward Moringe sokoine na kutoa ahadi ya kuwakaribisha mwaka kesho kushiriki maadhimisho ya miaka 30 toka hayati Edward Moringe Sokoine afariki dunia. Mgeni rasmi mwakani atakuwa Mh. rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dr. Jakaya Kikwete na mbio zitakuwa za kilomita 42.
Sikiliza Sauti ya Namelok Moringe Sokoine Hapa

No comments:

Post a Comment