UZIMAJI WA MITAMBO YA ANALOJIA ARUSHA NA MOSHI, ITAZIMWA TAREHE 31 MACHI 2013 - Wazalendo 25 Blog

Habari Mpya

Glory to Story.


Post Top Ad


28 Mar 2013

UZIMAJI WA MITAMBO YA ANALOJIA ARUSHA NA MOSHI, ITAZIMWA TAREHE 31 MACHI 2013


JAMHURI YA MUUNGANO WA TANZANIA
TAARIFA KWA VYOMBO VYA HABARI
UZIMAJI WA MITAMBO YA KURUSHA MATANGAZO YA TELEVISHENI YA MFUMO WA UTANGAZAJI WA ANALOJIA ARUSHA 31 MARCH 2013
Uzimaji wa mitambo ya utangazaji wa Televisheni ya mfumo wa analojia ulianza kutekelezwa tarehe 31/12/2012 saa sita kamili usiku katika jiji la Dar es Salaam kwa makubaliano ya nchi wanachama wa Jumuiya ya Afrika Mashariki. Uzimaji wa mitambo ya analojia umefinyika pia katika niji ya Dododma na Tanga tarehe 31/01/2013 na Mwanza tarehe 31/02/2013.
Kulingana na ratiba iliyotolewa na serikali mnamo mwezi desemba 2012 ,miji inayofuatia kuzima mitambo ya analojia ni Moshi na Hapa Arusha.
Maandalizi ya kuzima mitambo ya nalojia ya utangazaji wa televisheni kwa Arusha , yamekamilika kwa kushiriikiana na wadau wa sekta ya utangazaji hapa Arusha. Mitambo itazimwa saa sita kamili usiku.
Elimu kwa umma kupitia mbinu mbalimbali kuhusu mchakato wa kuhamia katika teknolojia ya mfumo wa utangazaji wa dijitali imekuwa ikitolewa kwa kiwango cha kuridhisha. Matangazo ya dijitali yanawafikia watu asilimia zaidi ya 20% kati a watu asilimia 24% wanaopata matangazo ya televisheni ya analojia .
Serikali ilifikiria kwa kina zoezi zima la kuzima mitambo ya televisheni ya teknolojia ya analojia kwa makini sana. Ili kufanikisha zoezi hili bila kuwa na usumbufu mkubwa ,serikali iliweka ratiba ya uzimaji kama ifuatavyo:
  1. Dar es Salaam – 31 Desemba 2012; Tayari mitambo ilishazimwa
  2. Dodoma & Tanga – 31 Januari ,2013 :Tayari mitambo imeshazimwa
  3. Mwanza – 28 Februari ,2013 ; tayari mitambo ilishazimwa
  4. Arusha & Moshi – 31 Machi ,2013; mitambo itazimwa
  5. Mbeya – 30 Aprili ,2013; mitambo itazimwa
Kama ilivyoolezwa tangu awali,utaratibu wa kuzima mitambo ya analojia utakuwa kwa maeneo yenye matangazo ya digitali tu. Maeneo ambayo hayana miundombinu ya dijitali hayatazimwa kwa sas hadi yapate dijitali.
Mabadiliko haya hayahusu matangazo kwa njia ya utangazaji wa  Sarelaiti , waya (cable) na Redio. Tunawataka wananchi wa Mkoa wa Arusha wasitupe TV zao za analojia bali wanunue ving’amuzi ili kupata matangazo ya dijitali.
Mamlaka ya Mawasiliano imeagiza watoa huduma za kusambaza ving’amuzi walioko Arusha kuhakikisha kuwa kunakuwa na Ving’amuzi vya kutosha. Tumefanya ukaguzi katika mji wa Arusha na tumehakikisha vuko ving’amuzi vya kutosha na tumehakikishiwa kuwa vingine viko njiani kuja mjini Arusha kati ya leo au kusho ambako zaidi ya ving’amuzi zaidi ya 5000 vitakuwa madukani.
Serikali inatarajia kupata ushiriakiano wa karibu kutoka kwa wadau wa sekta ya utangazaji na wananchi kwa ujumla katika kipindi cha uzimaji wa mitambo ya utangazaji wa televisheni ili kufanikisha zoezi la uzimaji wa mitambo ya utangazaji ya teknolojia ya analojia.

Imetolewa na:
Mkurugenzi Mkuu
Mamlaka ya Mawasiliano Tanzania (TCRA)
Machi 27,2013 – ARUSHA.

No comments:

Post a Comment

Post Top Ad