Na Lydia Churi- MAELEZO
Serikali imewasimamisha kazi na itawafungulia mashtaka ya kijeshi Maafisa watano wa Jeshi la Polisi nchini kutokana na tuhuma mbalimbali za ukiukaji wa maadili na taratibu za jeshi hilo.
Serikali imewasimamisha kazi na itawafungulia mashtaka ya kijeshi Maafisa watano wa Jeshi la Polisi nchini kutokana na tuhuma mbalimbali za ukiukaji wa maadili na taratibu za jeshi hilo.
Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi
Dkt. Emmanuel Nchimbi (pichani kulia) amewataja waliosimamishwa kazi
kuwa ni Elias Mwita aliyekuwa Mkuu wa Upelelezi Mkoa wa Mbeya, Jacob
Kiango aliyekuwa Msaidizi wa Mkuu wa Upelelezi Mkoa wa Mbeya na Charles
Kinyongo aliyekuwa Mkuu wa kikosi cha kutuliza Ghasia Mkoa wa Mbeya.
Dkt. Nchimbi amesema leo jijini
Dar es salaam kuwa viongozi hao wamesimamishwa kazi tangu jana kutokana
na kukiuka maadili ya jeshi la Polisi nchini ambapo wanatuhumiwa kwa
madai kuwa walipeleka chumvi na sukari kwenye Ofisi ya Mkemia Mkuu
badala ya kilo 1.9 ya madawa ya kulevya aina ya Cocaine yaliyokamatwa na
askari mkoani Mbeya mwezi Machi mwaka jana.
Waziri Nchimbi alisema vitendo
hivyo vinavyofanywa na viongozi wa jeshi la Polisi vinawavunja moyo na
kuwapa hofu askari wa ngazi ya chini ambao hushindwa kufanya kazi zao
kwa uadilifu unaotakiwa.
Katika hatua nyingine, aliyekuwa
mkuu wa Upelelezi mkoani Kagera Peter Matagi amesimamishwa kazi na
atafunguliwa mashtaka ya kijeshi kutokana na kukiuka taratibu za kazi
kwa kuwabambikiza kesi zisizo na dhamana wananchi 13 wa kata ya
Nyakasimbi wilaya ya Karagwe mkoa wa
Kagera Kutokana na vurugu za kugombea ardhi ambazo hazikuwiana na aina ya mashtaka walioshtakiwa hali inayoonesha dalili ya uwepo wa rushwa
Kagera Kutokana na vurugu za kugombea ardhi ambazo hazikuwiana na aina ya mashtaka walioshtakiwa hali inayoonesha dalili ya uwepo wa rushwa
Waziri Nchimbi alisema wananchi
hao walibambikizwa kesi ya ujambazi wa kutumia silaha ambapo walikaa
mahabusu kwa muda wa miezi miwili na baadaye timu ya uchunguzi
iliyoongozwa na waziri mwenyewe kugundua kuwa mashtaka waliyoshtakiwa
hayakuwa sahihi hali ambayo
ilisababisha Mwendesha Mashtaka Mkuu wa Serikali (DPP) aliifuta kesi.
ilisababisha Mwendesha Mashtaka Mkuu wa Serikali (DPP) aliifuta kesi.
Aidha, Serikali pia imemsimamisha
kazi aliyekuwa Mkuu wa Polisi wilaya ya Serengeti Paul Mng’ong’o kwa
kosa la kuingia katika Hifadhi ya Mbuga za wanyama ya Serengeti na
kupanga njama ya kuchimba madini aina ya dhahabu ndani ya hifadhi hiyo
hali iliyosababisha kiongozi huyo kushtakiwa kwenye mahakama ya kiraia
huko Serengeti.
Wakati huo huo Kamishna Msaidizi Mwandamizi wa Polisi aliyekuwa anasimamia ajira katika jeshi hilo nchini Renatus Chalamila amepewa likizo
ya mwezi mmoja baada ya kutajwa mara nyingi kuhusika na kuwatoza fedha vijana walioomba ajira ya jeshi la polisi ili awapatie kazi hiyo.
ya mwezi mmoja baada ya kutajwa mara nyingi kuhusika na kuwatoza fedha vijana walioomba ajira ya jeshi la polisi ili awapatie kazi hiyo.
Alisema Chalamila amepewa likizo hiyo na mapendekezo kupelekwa kwa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kama mamlaka ya nidhamu ili Rais afanye maamuzi juu ya tuhuma zinazomkabili askari huyo.
Kufuatia hali hiyo jeshi la polisi
limelazimika kuwaondoa katika mafunzo askari wanafunzi 95 waliokuwa
wamejiunga na chuo cha polisi baada ya kubainika kuwa walipata fursa
hiyo kwa kutoa fedha.
Waziri Nchimbi alitoa wito kuwa
Serikali itawaunga mkono askari wanaofanya kazi kwa uadilifu ila
watakaoenda kinyume na maadili na taratibu za jeshi la polisi serikali
haitasita kuwachukulia hatua za kisheria ikiwemo kuwafukuza kazi.
Hatua zilizochukuliwa na Serikali
kwa viongozi wa jeshi la polisi ni sehemu ya makubaliano ya Maafisa
waandamizi wa jeshi la Polisi nchini waliokutana hivi karibuni mjini
Dodoma kulinda maadili ya jeshi hilo na kukabiliana na vitendo vyote
vinavyolichafua jeshi hilo kwa jamii ili kutatua kero za wananchi na
kuzingatia utawala bora.
No comments:
Post a Comment