Taarifa kutoka kituo cha Sheria
na Haki za Binadamu (LHRC) zilizotumwa katika mitandao ya Kijamii na Bi Hellen
Kijo bisimba mchana huu zinapasha kuwa kuzuka vurugu na kusababisha majeruhi
huko Wilayani Chato.
Tumepokea taarifa za
masikitiko kuhusu vurugu zilizotokea huko Buselele Chato kuhusu uchinjaji wa
nyama unaobishaniwa na Waislam na Wakristo.
Chanzo cha Habari hizi
kimetueleza kuwa baada ya mivutano kuhusu uchinjaji wa nyama .Baaadhi ya
Wakristo waliamua kuanzisha bucha ya ili wachinje na kununua hapo ili
wasishiriki kula nyama zilizochinjwa kama sehemu ya ibada ya Kiislamu kwa vile
uchinjaji kwa Waislam ni ibada.
Baada ya kufungua Bucha hiyo
leo asubuhi taarifa inasema watu wanaosadikiwa kuwa waislam walifika kutaka
kuifunga hiyo Bucha na baadaye Polisi nao walifika na walitaka wamchukue mwenye
bucha hiyi .
Suala hili likazua tafrani na
pakatokea mapigano kati ya pande mbili yaani waislam na wakristo na kuna watu
wameumizwa.Taarifa imezidi kueleza kuwa pia mali za aliyehamasisha ufungwaji wa
bucha nazo zimeharibiwa. Baada ya kupokea taarifa hii tumewatuma waangalizi
wetu wa haki za binadamu kwenda kutuletea kwa kina hali halisi kama watakavyoweza.
Tunahabari kuwa kikosi cha
kuzuia fujo kilifika na kutuliza hizo vurugu.Jambo tunaloliona kwa haraka ni
kuwa kunaelekea kukosekana kwa uongozi wa kuyatazama masuala kama haya na
kuyawekea msimamo na maelekezo kabla vurugu kama hizi kutokea.
Pili tunaona kuwa hali ya
kukosa stahamala za kidini inajengeka nchini jambo ambalo ni hatari sana kwa
usalama na amani hapa nchini.Wakati tunasubiri taarifa zaidi tunapenda kutoa
angalizo kwa viongozi wetu maana tumesikia mkuu wa wilaya tayari ameshafika
katika eneo la tukio.
Masuala kama haya yatazamwe
kwa mujibu wa sheria na sheria zifuatwe lakini pia kwa kuzingatia haki za
binadamu na hususani haki za kiraia na kiutamaduni ambazo zinatoa uhuru wa
ibada na kila mtu asiingiliwe katika haki hizi.
Lakini pia njia za utatuzi wa
migogoro ya aina hii isifanywe kijuujuuu bali pawe na nafasi yamaongezi ya kina
ya uchambuzi wa kiini cha mgogoro. Tutaweza kutoa taarifa zaidi tutakapopokea
taarifa kutoka kwa waangalizi wetu wa kiini na matokeo ya mgogoro au vurugu
hizi. Source Father Kidevu blog
No comments:
Post a Comment