Bishop Thomas O. Laizer .
FAMILIA ya marehemu
Baba Askofu Thomas Laizer wa Kanisa la kiinjili la kilutheri Tanzania
dayosisi ya kaskazini kati imesema kuwa hayati Baba askofu ameacha wosia mzito
kwa waumini, wachungaji na viongozi wa kanisa hilo baada ya yeye kupita.
Akizungumza nyumbani kwa askofu huyo katika eneo la Nduruma
mke wa askofu huyo Mama Maria Laizer alisema kuwa mume wake kila mara alikuwa
anasisitiza kuwa kazi aliyoianzisha iendelezwe na isiharibiwe kwa vyovyote
vile.
“Baba askofu alisisitiza
jambo hili hata kwa wote waliofika kumjulia hali akiwa kitandani kwake kuwa
wahakikishe kuwa kazi aliyoianza inaendelezwa “alisema Mama Laizer.
Alileza kuwa alikuwa na mume wake masaa machache kabla ya
kifo chake na kwamba mchana wa siku aliyoaga dunia alikuwa na hali nzuri lakini
baadye hali yake ilibadilika na kuondokewa na uhai.
Alisema kuwa askofyu huyo alianza kusumbuliwa na maradhi ya
kansa kwa kipindi cha miaka minne iliyopita lakini hakuweza kupata tiba stahili
kwa haraka.
“Alikuwa akilalamika maumivu katika tumbo lake mara kwa mara
na baadaye alizidiwa tukampeleka Nairobi akatibiwa lakini baada ya muda alianza
tena kulalamika maumvu na ndipo akapelekwa India na kugundulika kuugua kansa
ambayo tayari ilikuwa imesambaa mwilini”alisema Mama Laizer.
Marehemu Baba askofu Thomas Laizer ameacha mjane watoto wanne
na mjukuu mmoja.
RATIBA YA MAZISHI
Hatimaye mwili wa askofu wa Kanisa la Kilutheri
Tanzania (KKKT) Dayosisi yaKaskazini Kati,Marehemu Askofu Dk. Thomas Laizer unatarajiwa
kuzikwa Ijumaa ya wiki ijayo Februari 15, 2013.
Taarifa
iliyotolewa na Kamati ya Mazishi ya KKKT na Familia ya Marehemu, imeeleza kuwa
Marehemu atazikwa katika eneo la Kanisa Kuu mjini Kati Jijini Arusha.
Aidha taarifa
hiyo inasema kuwa waumini na Washirika wa Kanisa Kuu na makanisa yote ya KKKT
nchini, Wananchi, ndugu jamaa na marafiki watapata fursa ya kutoa heshima zao
za mwisho kwa Mwili wa marehemu kuanzia siku
ya Alhamisi mchana ya Februari 14, 2013.
Taarifa hiyo
iliongeza kuwa Mwili wa Askofu Laizer utalala Kanisani hapo hadi Ijumaa ya
Mazishi.
Marehemu Askofu
Thomas Laizer aliyezaliwa Machi 10, 1945 katika Kijiji cha Kitumbeine Wilayani Longido na
baade kupata elimu yake ya msingi hadi darasa la nane Longido na kumaliza mwaka
1965.
Askofu Laizer,
aliendelea na masomo yake ya juu ndani na baade kujiunga na masomo ya Theolojia
katika chuo cha Makumira na baadae kuongeza masomo nchini Marekani.
Marehemu wakati
wa uhai wake alikuwa Mwinjilisti, Mchungaji katika makanisa mbalimbali nchini
na baadae kuwa Mkuu wa Jimbo na Mkuu wa Sinodi na baadae kuwa Rais wa sinodi
kabla ya kusimikwa rasmi kuwa Askofu wa Kwanza wa Dayosisi ya Arusha ambayo kwa
sasa ni Dayosisi ya Kaskazini Kati. Kwa maelezo zaidi bofya hapa >>>
|
DC MKUDE AVITAKA VYAMA VYA MSINGI VYA USHIRIKA AMCOS KUTOA ELIMU KUHUSU
PAMBA
-
Mkuu wa Wilaya ya Kishapu, Mkoani Shinyanga, Mhe. Joseph Mkude
Na Sumai Salum - Kishapu
Mkuu wa Wilaya ya Kishapu, Mkoani Shinyanga, Mhe. Joseph Mkude, am...
3 hours ago
No comments:
Post a Comment