Kaimu Mkurugenzi wa Biashara, Bi. Mwanamvua Ngocho, akizungumuza
na wageni waalikwa, abiria waliosafiri na ndege la shirika hilo, pamoja
na maofisa wa uwanja wa ndege la Mtwara (hawapo pichani) wakati wa
uzinduzi wa safari za ndege za Shirila la Ndege la Tanzania (ATCL)
mkoani Mtwara , mara tu baada ya kutua ndege hiyo uwanjani hapo mwishoni
mwa wiki.
Meya
wa Mtwara Mikindani, Selemani Mtalika Shilingi ambaye alikuwa mgeni
rasmi wakati wa uzinduzi wa safari za ndege za Shirila la Ndege la
Tanzania (ATCL) mkoani Mtwara, akizungumuza na wageni waalikwa, abiria
waliosafiri na ndege la shirika hilo, pamoja na maofisa wa uwanja wa
ndege la Mtwara (hawapo pichani) mara tu baada ya kutua ndege hiyo
uwanjani hapo mwishoni mwa wiki. Kushoto ni Kaimu
Mkurugenzi wa Biashara, Bi. Mwanamvua Ngocho na kulia ni Meneja
Rasilimali watu na Utawala, Bi. Halima Nabalang’anya. Picha na mwandishi
wetu.
Baadhi ya
abiria waliopanda dege ya Shirika la ndege la Tanzania (ATCL),
wakitembea kuelekea katika chumba cha kupumzikia abirai, wakati wa
uzinduzi wa safari za ndege za shirila hilo mkoani Mtwara iliyofanyika
mwishoni mwa wiki.
====== ====== ========
Safari za ndege ya ATCL kwenda Mtwara zaanza
Na Mwandishi Wetu
SHIRIKA la Ndege
la Air Tanzania (ATCL) mwishoni mwa wiki lilizindua upya safari zake za
moja kwa moja za Dar es Salaam-Mtwara na kuahidi kuongeza idadi ya
safari hizo na kutoza nauli nafuu.
Akizungumza baada ya
kutua katika uwanja wa ndege wa Mtwara, Kaimu Mkurugenzi wa Biashara,
Bi. Mwanamvua Ngocho alisema kuwa kurejeshwa kwa huduma za usafiri wa
anga na shirika hilo la taifa mjini Mtwara ni chachu ya mapinduzi
makubwa katika usafiri wa anga mjini hapo kwa kuhakikisha kuwa abiria
wanapata huduma bora na za kiushindani.
"Nataka
kuwahakikishia wakazi wa Mtwara kwamba ndege yao ya taifa imekuja
kuwahudumia watu wa mkoa huu. Kwa kuanzia, tutaruka Mtwara mara nne
katika wiki; ikiwa ni siku za Jumatatu, Jumatano, Ijumaa na Jumapili,
lakini tutaendelea kufanya marekebisho ya safari kutegemeana na
mahitaji. Abiria watarajie ATCL kuwapatia huduma ambazo ni salama na za
gharama nafuu, "alisema.
Mwanamvua alieleza
kuwa shirika hilo litatoza shilingi 199,000 / - kwa tiketi ya kwenda na
kurudi, na kuahidi kuwa shirika hilo litafanyia kazi suala la kupunguza
gharama za usafiri zaidi ili kuwawezesha wasafiri wanaoenda na kutoka
Mtwara kuona faida za kutumia usafiri wa anga.
Kwa upande wake, Meya wa Mtwara
Mikindani, Selemani Mtalika Shilingi ambaye alikuwa mgeni rasmi, alisema
baada ya ndege ya taifa kurejesha huduma zake mkoani Mtwara, wakati wa
shirika moja la ndege kutawala utoaji huduma mkoani hapo na kulazimisha
abiria kulipa nauli za juu, sasa umekwisha.
“Ninafuraha kuona shirika la ndege
la taifa likiwa limerejesha huduma zake mkoani Mtwara. Kwa muda mrefu
sasa usafiri wa anga hapa Mtwara imekuwa ikitawaliwa na shirika moja tu
la ndege. Ukweli ni kwamba, pasikuwepo na ushindani, suala la bei mara
nyingi ni changamoto kwa walaji/wateja. Abiria wa kwenda na kutoka
Mtwara wamekuwa wakilipa nauli za juu. Ila kwa kuwa tuna ATCL sasa na
Kaimu Mgurugenzi wa Biashara ametuakikishia, wakazi wa Mtwara na wageni
wetu watapata fursa ya kufurahia usafiri wa anga ulio salama na wa
gharama nafuu,” alisema Shilingi.
Meya huyo alisema kuwa idadi ya
abiria wanaokwenda Mtwara imekuwa ikiongezeka sana katika siku za
karibuni, kwa sababu Mtwara imekuwa na sura ya kibiashara baada ya
ugunduzi wa kiasi kikubwa cha gesi asilia na kuwa mkoa unaozalishaji zao
la korosho kwa wingi hapa nchini.
“Wawekezaji wengi wanaendelea
kumiminika katika mkoa wetu, na hivi karibuni Mtwara itakuwa na
muonekano tofauti kabisa. Ushawishi huu wa kuwekeza mkoani Mtwara
umeongeza idadi ya abiria wanaosafiri na ndege. Nina uhakika ATCL itaona
ongezeko la abiria mapema na kulifanya shirika kuongeza idadi ya safari
zake mapema,” alisema.
Shirika hilo litatumia ndege yake
aina ya Dash 8-300 yenye uwezo wa kubeba abiria 50, wakati huu wa
mwanzoni, lakini uongozi umebainisha kuwa pale idadi ya abiria
itakapoongezeka kuzidi uwezo wa Dash 8, watatumia ndege yao aina ya
Boeing.
Urejeshwaji wa safari za Mtwara
umekuja ikiwa ni mwezi mmoja tu baada ya shirika hilo pia kurejesha
safari za Kigoma baada ukarabati wa uwanja wa ndege wa Kigoma
kumalizika.
No comments:
Post a Comment