KOCHA WA MCHEZO WA RIADHA BW. SAMWEL TUPPA AKIWANOA VIJANA WAKE - Wazalendo 25 Blog

Glory to Story.

Habari Mpya

PRINTING / GRAPHICS / DESIGN : 0784 643 633


PRINTING / GRAPHICS / DESIGN : 0676 643 633

Tuesday, 19 February 2013

KOCHA WA MCHEZO WA RIADHA BW. SAMWEL TUPPA AKIWANOA VIJANA WAKE

Kocha Mkongwe wa mchezo wa Riadha Bw. Samwel Tuppa akiwa katika uwanja wa mpira wa Sheikh Amri Abeid  jijini Arusha, akiwafundisha mazoezi mbalimbali ya kuruka wanamichezo na washindi wa medali za mchezo huo kitaifa na Kimataifa.

Kocha Tuppa akiongea na ASILI YETU TANZANIA amesema kuwa yuko katika harakati za kuwanoa vijana wake ili hivi karibuni waweze kuungana na timu ya Taifa ya mchezo huo katika michezo ya kitaifa itakayokuwa ikifanyika hivi karibuni.

Huyu ni mshindi wa kitaifa wa medali nne Bw. Michael Danford, akiwa katika mazoezi na kocha wake Samwel Tuppa katika uwanja wa Sheikh Amri Abeid jijini Arusha.
  

Samwel Tuppa ni kocha wa Kimataifa wa Riadha na anae tambulika na chama cha riadha cha Dunia (IAAF) . ni mzoefu sana na anatarajia kutoa vijana ambao wataiwakilisha nchi ya Tanzania kitaifa na kimataifa katika nyanja mbalimbali ya Riadha,ila ameelezea changamoto zinazomkabaili.

Tupa ameeleza changamoto nyingi zinazowakabili wachezaji wake, kuwa ni wadhamini kutojitokeza kuwaunga mkono na kuwawezesha kukidhi mahitaji ya vifaa mbali mbali  vya mazoezi na kuwasaidia kushiriki mashindano mbali mbali ya kitaifa na kimataifa.
Ni wito kwa watanzania kujitokeza kuwawezesha wachezaji hawa na washindi wa medali za mchezo wa kuruka nchini, kwani wana uwezo mkubwa wa kushiriki na kunyakua medali zaidi ya hizo nje ya nchi na kuweza kuitangaza Tanzania kimataifa.

Mshindi wa kitaifa wa medali nne katika mchezo wa kuruka Bw. Micahel Danford, akiwa katika mazoezi ya mchezo huo katika uwanja wa Sheikh Amri Abeid jijini Arusha.
Hapa Kijana Michael Danford ,akiruka viunzi kwa ustadi wa hali ya juu, katika uwanja wa Sheikh Amri Abeid Jijini Arusha.

No comments:

Post a Comment