Mkurugenzi
wa Biashara wa CFAO Motors Wayne Mcintosh akizindua rasmi gari ya
Nissan Patrol aina ya Y62 leo katika makao makuu ya kampuni hiyo jijini
Dar es Salaam. Katika
uzinduzi huo wa gari hiyo mpya ambayo ni Four Wheel Drive yenye uwezo
wa kubeba watu 8 na yenye nguvu ya 5.6L V8 injini yenye spidi ya 240 ni
ya pekee duniani kuzinduliwa na Tanzania inakuwa ya kwanza katika nchi za Afrika Mashariki na kati kuingia baada ya Congo DRC, Angola na Ghana. Bw. Mcintosh amesisitiza kwamba gari hii inaviburudisho pamoja na Tv katika hali ya kumsaidia dereva kwenye safari ndefu.
Baadhi ya wafanyakazi wa Kampuni ya CFAO Motors na wageni waalikwa
wakimsikiliza Bw. Wayne Mcintosh (hayupo pichani) kwenye uzinduzi huo.
Meneja Masoko wa Kampuni ya CFAO Motors Tharaia Ahmed (wa pili kulia) na baadhi ya wageni waalikwa.
Mkurugenzi
wa Biashara wa CFAO Motors Wayne Mcintosh akiendesha bahati nasibu ya
kwenda kushuhudia fainali na Michuano ya kombe la Mataifa barani Afrika
inayofanyika nchini Afrika kusini kwa wageni waliohudhuria uzinduzi huo.
Mkurugenzi
wa Biashara wa CFAO Motors Wayne Mcintosh akitangaza washindi wawili
watakaoenda nchini Afrika Kusini kushuhudia fainali za mashindano ya
AFCON.
Mkurugenzi wa Biashara wa CFAO Motors Wayne Mcintosh akimpongeza mshindi wa shindano la bahati nasibu Group Manager wa DELFINA Bw. Sajjad Dharamsi atakayeenda
nchini Afrika Kusini kushuhudia fainali za mashindano ya michuano ya
AFCON 2013. Kushoto ni Meneja Masoko wa CFAO Motors Tharaia Ahmed.
Bw. Wayne Mcintosh akimpongeza mshindi wa pili wa Kampuni ya Wambi Lube Oil Distributor Bw. Omari Omari.
Peer Educator wa CFAO Motors Maria
Petro (kulia) akimpongeza Bw. Omari Omari kwa kushinda droo ya kwenda
kutizama fainali za AFCON 2013 nchini Afrika Kusini iliyoendeshwa na
kampuni hiyo wakati wa hafla ya uzinduzi wa gari mpya aina ya Nissan
Patrol Y62. Katikati ni Meneja Masoko wa CFAO Motors Tharaia Ahmed.
Afisa
Mauzo wa CFAO Motors Magdalena Mpeku akitoa maelezo ya gari mpya aina
ya Nissan Patrol Y62 kwa baadhi ya wageni waalikwa waliohudhuria
uzinduzi huo. kwa picha zaidi bofya hapa>>>
No comments:
Post a Comment