|
Mwanaharakati wa Michezo ya Riadha nchini Bw. Wilhelm Gidabuday. |
Rais wa TFF,Leodger Tenga
*********************************
Na
Gadiel Urio - Arusha
Mwanaharakati
, mzalendo na mwanariadha wa kimataifa
na mdau mkubwa wa michezo nchini Bw. Wilhem GidaBuday amempogeza raisi wa TFF
nchini Bw. Leodgar C. Tenga na kusema
kitendo alichokifanya ni cha kizalendo, cha kitaifa na kinafaa kuigwa na
viongozi wengine wa michezo nchini.
Bw Gidabuday aliongeza kuwa Raisi wa TFF
ameionyesha jamii ya kitanzania kuwa yeye sio mbinafsi ,sio mchoyo wa madaraka na
anapenda maendeleo ya wa Tanzania wengine
,ndio maana akaachia kiti hicho ili kiweze kuongozwa na wadau wengine wa
michezo nchini.
“Leodgar Tenga amefanya uamuzi wa kizalendo,kiungwana,kitaifa na wa
kuigwa. Imethibitika kuwa Tenga hana ubinafsi; tofauti na wenzetu wa TOC ambao
walikuwa tayari hata kuua mtu ili kuhakikisha kuwa wanashinda!!Tukumbuke kwamba
katiba zetu za vyama vya michezo vimeundwa na walafi ambao wame – Monopolize vyama
vya michezo kuwa mali zao binafsi!.
Mfano: Olympic Movement ina objective zake
mahususi kama vile Usawa, Haki, Maadili ya kiutu,Kupinga Ubaguzi na
Ufisadi!!.But guess what; TOC ndo wanaendesha mambo kinyume kabisa na IOC’s
code of Ethics na serikali inawaogopa! hadi lini?”. Alihoji na kumalizia mwanaharakati
huyo wa michezo hususani mchezo wa Riadha nchini Bw. Wilhelm Gidabuday
No comments:
Post a Comment