Mtandao wa Jinsia Tanzania (TGNP) wakutana na Tume ya Katiba - Wazalendo 25 Blog

Glory to Story.

Habari Mpya

PRINTING / GRAPHICS / DESIGN : 0784 643 633


PRINTING / GRAPHICS / DESIGN : 0676 643 633

Thursday, 10 January 2013

Mtandao wa Jinsia Tanzania (TGNP) wakutana na Tume ya Katiba

Mwenyekiti wa Tume ya Mabadiliko ya Katiba Jaji Joseph Warioba akiongea katika mkutano na Mtandao wa Jinsia Tanzania (TGNP) uliolenga kupata maoni ya mtandao huo kuhusu Katiba Mpya , katika ofisi za Tume jijini Dar es Salaam. Kulia kwa Jaji Warioba ni Bi. Ussu Mallya, Mkurugenzi Mtendaji wa mtandao huo, Prof. Ruth Meena Mjumbe wa Bodi ya TGNP) na Mwenyekiti wa TGNP Bi. Mary Rusimbi.
Mjumbe wa Tume ya Mabadiliko ya Katiba Dkt. Sengondo Mvungi akiongea katika mkutano na Mtandao wa Jinsia Tanzania (TGNP) uliolenga kupata maoni ya mtandao huo kuhusu Katiba Mpya, katika ofisi za Tume jijini Dar es Salaam. Kushoto kwake ni Wajumbe wengine wa Tume Bi. Mary Kashonda na Bi. Salma Moulidi.
Mwananchama wa Mtandao wa Jinsia Tanzania (TGNP) Bi. Subira Kibiga akitoa maoni ya mtandao huo kuhusu Katiba Mpya katika mkutano na Tume ya Mabadiliko ya Katiba , katika ofisi za Tume jijini Dar es Salaam. Wengine ni wananchama wenzake Bi. Diana Mwiru (kushoto) na Bi. Asseny Muro.
Mwanachama wa Mtandao wa Jinsia Tanzania (TGNP) Bi. Asseny Muro akitoa maoni ya mtandao huo kuhusu Katiba Mpya katika mkutano na Tume ya Mabadiliko ya Katiba Mpya, katika ofisi za Tume jijini Dar es Salaam. Kulia kwake ni Mwenyekiti wa TGNP Bi. Mary Rusimbi na Mjumbe wa Bodi ya mtandao huo Prof. Ruth Meena.
Baadhi ya Wajumbe ya Mabadiliko ya Katiba katika picha ya pamoja na Wanachama na viongozi wa Mtandao wa Jinsia Tanzania (TGNP) mara baada ya mtandao huo kuwasilisha maoni yake kuhusu Katiba Mpya , katika ofisi za Tume jijini Dar es Salaam). na Lukaza Blog

No comments:

Post a Comment