MAMA SALMA KIKWETE AWAFANYIA SHERRY PARTY WENZA WA MABALOZI DAR ES SALAAM - Wazalendo 25 Blog

Glory to Story.

Habari Mpya

PRINTING / GRAPHICS / DESIGN : 0784 643 633

Wednesday, 16 January 2013

MAMA SALMA KIKWETE AWAFANYIA SHERRY PARTY WENZA WA MABALOZI DAR ES SALAAM


 Mke wa Rais Mama Salma Kikwete (kushoto) akisalimiana na Mdau Fauzia Aboud katika hafla hiyo katika viwanja vya Ikulu jijini Dar e Salaam Jan15,2013.
 Baadhi ya wake wa Mabalozi wanaowakilisha nchi zaoTanzania wakisubiri kuanza kwa hafla ya kukaribisha mwaka mpya2013 katika viwanja vya Ikulu jjijini Dsm Jan 15,2013 iliyoandaliwa na Mke wa Rais Mama Salma Kikwete (hayupo pichani).
Mke wa Rais Mama Salma Kikwete (mwenye kilemba) akipongezana na Kiongozi wa wenza wa Mabalozi nchini Celine Khalfan Juma Mpango katika hafla ya kusherehekea na kukaribisha mwaka mpya 2013 katika viwanja vya Ikulu jijini Dar es Salaam Jan 15,2013.
 Mke wa Rais Mama Salma Kikwete(mwenye kilemba)akipongezana na Consulate wa Jamhuri ya Poland Bibi Grazyna Tairo kwenye hafla ya kuwakaribisha wenza wa Mabalozi nchini jan 15,2013 katika viwanja vya Ikulu jijini Dar es Salaam.
 2-Mke wa Rais Mama Salma Kikwete (mwenye kilemba) akibadilishana mawazo na baadhi ya wenza wa Mabalozi wanaowakilisha nchi zao nchini wakati wa sherehe ya hafla ya kuukaribisha miaka 2013 katika viwanja vya Ikulu jijini Dar es Salaam,jan 15,2013.
 Mke wa Rais Mama Salma Kikwete akiongea kwenye hafla maalumu ya kuwakaribisha wake wa Balozi nchini kwa mwaka mpya 2013, Hafla hiyo imefanyika katika viwanja vya Ikulu jijini Dar- es Salaam , Jan 15,2013.
 Mke wa Makamu wa Rais Mama Asha Bilal (kushoto) akibadilishana mawazo na Mke wa Waziri Mkuu Mama Tunu Pinda (kulia) katika hafla maalumu ya mwaka mpya 2013 kwaajili ya wake wa Mabalozi iliyoandaliwa na Mke wa Rais Mama Salma Kikwete(hayupo pichani) kwenye viwanja vya Ikulu jijini Dar es Salaam Jan,15,2013.
Mke wa Rais Mama Salma Kikwete akisalimiana na Mke wa Rais Mstaafu Mama Sitti Mwinyi(kushoto) katika hafla mwaka mpya2013 ya kuwakaribisha (SPOUSE) wake wa Mabalozi nchini Jan 15,2013 katika viwanja vya Ikulu jijini Dar es Salaam,( Picha zote na Mwanakombo Jumaa-MAELEZO).
Pix no 7-Mke wa Makamu wa Rais Mama Asha Bilal (aliekaa) akisalimiana na Msaidizi Mwandamizi wa Rais masuala ya Diplomasia , Liberata Mulamula walipokutana katika halfa ya kusherehekea mwaka mpya 2013 kwaajili ya wake wa Mabalozi nchini iliyoandaliwa na Mke wa Rais Mama Salma Kikwete katika viwanja vya Ikulu jijini Dar es Salaam Jan 15,2013,

No comments:

Post a Comment