Muonekano wa Jengo la Uhuru Heights lililopo barabara ya Bibi Titi Mohammed liking'arisha jiji la Dar nyakati za usiku.
MC katika uzinduzi wa Jengo la Uhuru Heights Taji Liundi.
Mgeni
rasmi Balozi wa Pakistan nchini Tanzania Tajammul Altaf akipokea shada
la maua kutoka kwa watoto Ilsa na Alaisa ikiwa shukrani kwa kuhudhuria
sherehe za uzinduzi wa jengo la Uhuru Heights. Kushoto ni Mwenyekiti wa
Cosmos Group ambao ndio wamiliki wa jengo la Uhuru Heights Muhammad
Owasi Pardesi na wa pili kulia ni Afisa Mtendaji Mkuu wa International
Commercial Bank (Tanzania) LTD Basser Mohamed.
Ilsa na Alaisa wakiimba wimbo wa Taifa kubariki sherehe za ufunguzi wa jengo hilo.
Mgeni
rasmi Balozi wa Pakistan nchini Tanzania Tajammul Altaf akizungumza
katika uzinduzi huo ambapo amasema amefurahishwa na jitihada
zilizofanywa na mfanyabiashara kutoka nchini kwake na jinsi Tanzania
ilivyoweza kumpa ushirikiano na hatimaye sasa matunda yameonekana kwa
kuzaliwa jengo la Uhuru Heights lenye hadi ya Kimataifa.
Aidha
amesema huo ni mwanzo tu na kuwataka wafanyabiashara zaidi kutoka
Pakistan kuja kuwekeza Tanzania kwa sababu mahali ambapo ukiwekeza
matunda yanaonekana kutokana na amani na utulivu uliopo na ushirikiano
wa serikali.
Mwenyekiti wa Cosmos Group ambao ndio wamiliki wa jengo la Uhuru
Heights Muhammad Owasi Pardesi akizungumza na wageni wakati wa uzinduzi
wa jengo hilo na kutoa shukrani zake akisema sasa wakazi wa Dar es
Salaam wataweza kununua nyumba kwa njia ya mkopo kutoka Benki ya
International Commercial (ICB) na kulipa kwa muda wa miaka 10 na kuishi
katika miongoni mwa majengo marefu ya makazi yaliyopo katikati ya jiji
la Dar es Salaam lililojengwa kwa gharama ya Dola za Kimarekani Bilioni
40.
Amesema
Malengo ya kampuni ya Cosmos Group ni kuboresha miundo mbinu na maisha
ya watu na hayo yamezingatiwa kwa kujenga jengo la Uhuru Heights.
CEO wa VFX Dubai Yusuf Thakur akizungumza wakati wa uzinduzi huo.
Afisa
Mtendaji Mkuu wa International Commercial Bank (Tanzania) LTD Basser
Mohamed akielezea wageni waalikwa jinsi watakavyoweza kufaidika na
mikopo itakayotolewa na Benki hiyo ikiwemo kupata kipindi cha marejesho
ya mkopo kwa miezi 120, viwango nafuu vya riba, kiwango cha juu cha umri
wa mkopaji ni miaka 60 kufikia kipindi mkopo unapotolewa na mkopo huo
unapatikana kwa hela za madafu na dola za Marekani.
Mkurugenzi
Mkuu wa Benki ya EXIM Anthony Grant akifafanua namna wateja wa Benki ya
Exim watakavyoweza kunufaika na mkopo kwa ajili ya kununua nyumba
zilizopo katika jengo la Uhuru Heights.
Mwenyekiti wa Cosmos Group ambao ndio wamiliki wa jengo la Uhuru Heights Muhammad Owasi Pardesi akipeana mikono na Afisa Mtendaji Mkuu wa International Commercial Bank (Tanzania) LTD Basser Mohamed (katikati), Mkurugenzi Mkuu wa Benki ya EXIM Anthony Grant (kushoto) ikiwa ni ishara ya kuingia mkataba wa kufanya biashara pamoja baina ya Cosmos, IBC Benki na Exim.
CEO
wa VFX Dubai Yusuf Thakur akiendesha zoezi la mauzo ya nyumba katika
jengo la Uhuru Heights ambapo mteja wa kwanza Samantar Abdinur Iusuf
(kulia) aliyejitokeza kununua makazi katika jengo hilo.
Mgeni
rasmi Mh. Tajammul Altaf akimpongeza mteja wa kwanz baada ya kununua
moja ya nyumba kuashiria uzinduzi wa idara ya mauzo na wageni wengine
pia kuendelea na manunuzi wakati wa uzinduzi huo.
Balozi wa Japan nchini Tanzania Salome Sijaona ( wa pili kushoto)
akizungumza jambo la msingi wakati wakitembelea maeneo mbalimbali ya
jengo hilo na Mwenyekiti wa Cosmos Group ambao ndio wamiliki wa jengo la
Uhuru Heights Muhammad Owasi Pardesi. Kushoto ni mgeni rasmi Balozi
Tajammul Altaf.
Wasanii
wa kikundi cha ngoma za asili cha Safi Theatre wakitoa burudani wakati
wa uzinduzi wa jengo jipya la kisasa la biashara na makazi la Uhuru
Heights jijini Dar.
Waziri wa zamani Mh. Juma Ngasongwa akizungumza jambo na baadhi ya wageni waliohudhuria uzinduzi huo.
Mh. Mohammed Dewji akibadilishana mawazo na Waziri wa zamani Mh. Juma
Ngasongwa na wageni wengine wakati wa hafla ya uzinduzi wa jengo la
Uhuru Heights.
Mwenyekiti wa Cosmos Group ambao ndio wamililki wa jengo la Uhuru
Heights Muhammad Owasi Pardesi akibadilishana mawazo na baadhi ya wageni
waalikwa.
Pichani Juu na Chini ni baadhi ya wageni, viongozi wa Serikali na
wafanyabiashara wakubwa nchini waliohudhuria uzinduzi wa Jengo la Uhuru
Heights.
Mmoja wa wafanyakazi wa benki ya ICB wakitoa maelezo ya jinsi ya kupata mikopo ya nyumba kupitia benki hiyo.
Mgeni rasmi Balozi Tajammul Altaf na mwenyeji wake wakiwa ndani ya moja ya vyumba vya makazi ndani ya jengo hilo.
Balozi Tajammul Altaf akingalia muonekano wa mandhari ya jiji la Dar akiwa gorofa ya 12 ndani ya jengo jipya la Uhuru Heights.
Afisa
Mtendaji Mkuu wa International Commercial Bank (Tanzania) LTD Basser
Mohamed katika picha ya pamoja na wafanyakazi wa benki hiyo.
Wasichana warembo na watanashati wa Kitengo cha Mauzo cha Uhuru Heights wakipozi na mmoja wa wafanyakazi wa kampuni hiyo.
Pichani Juu na Chini ni Mwenyekiti wa Cosmos Group ambao ndio wamililki
wa jengo la Uhuru Heights Muhammad Owasi Pardesi katika picha ya
pamoja na wafanyakazi wa kampuni hiyo na waandaji wa uzinduzi huo.Picha na Mo Blog
No comments:
Post a Comment