Katibu
mkuu wa Wizara ya Viwanda na Biashara Bi. Joyce Mapunjo akizungumza na
wahitimu 2882 wa Chuo cha Elimu ya Biashara Dar es salaam (CBE) wakati
wa mahafali ya 47 ya Chuo hicho yaliyofanyika katika viwanja vya Mnazi
mmoja jana jioni Jijini Dar es salaam na kuwataka kutumia elimu yao
kujiajiri na kuwa chachu ya maendeleo nchini.
Kaimu
Mkuu wa Chuo cha Elimu ya Biashara Dar es salaam (CBE) Bw. Athman
Ahmed (kulia) akitoa taarifa kuhusu mahafali ya 47 na maendeleo ya chuo
hicho kwa mgeni rasmi wa mahafali hayo Katibu Mkuu wa Wizara ya Viwanda
na Biashara Bi. Joyce Mapunjo (katikati).
Baadhi
ya wahitimu wa shahada ya Masoko katika Chuo cha Biashara Dar es
salaam wakiweka kofia zao sawa mara baada ya kumalizika kwa tamko la
kuwatuku shahada hiyo.
Wahitimu
wa mahafali ya 47 ya Chuo cha CBE wakifuatilia masuala mbalimbali
yaliyokua yakiendelea wakati wa mahafali hayo katika viwanja vya Mnazi
mmoja jijini Dar es salaam.
Baadhi
ya wananchi na wapiga picha wa kujitegemea waliohudhuria mahafali ya 47
ya Chuo cha CBE sehemu ya Dar es salaam wakiendelea kufuatilia matukio
mbalimbali wakati wa sherehe hizo.(Picha na Aron Msigwa – MAELEZO).
Na. Aron Msigwa –MAELEZO.
Wahitimu
wa Chuo cha Elimu ya Biashara Dar es salaam wametakiwa kutumia fursa
na elimu waliyoipata wakati wa masomo yao kujiajiri wenyewe badala ya
kusubiri kuajiriwa ili kupunguza ongezeko kubwa la vijana wasio na ajira
mitaani.
Akizungumza
na wahitimu 2882 wa fani mbalimbali wa chuo hicho wakati wa mahafali ya
47 yaliyofanyika jana jioni jijini Dar es salaam, Katibu Mkuu wa Wizara
ya Viwanda na Biashara Bi. Joyce Mapunjo amewataka vijana hao kutumia
elimu yao kujiajiri wenyewe na kutengeza ajira kwa vijana wengine
wanaohangaika kutafuta kazi kila kukicha.
Amewataka
wahitimu hao kuwa mfano wa kuigwa katika jamii na kutumia elimu yao
kutatua matatizo mbalimbali yanayoikabili jamii na kuwaasa kujiepusha na
vitendo vya uhalifu, anasa na kujikinga na maambukizi ya VVU.
Kuhusu
kukisaidia chuo hicho Bi. Joyce amesema kuwa serikali itaendelea
kukisaidia chuo hicho kifedha ili kiweze kutimiza malengo mbalimbali
kiliyojiwekea na kutoa wito kwa viongozi wa chuo hicho kuongeza ubunifu
katika kutafuta vyanzo mbalimbali vya mapato ya chuo hicho.
Aidha
amesema kuwa ongezeko la wahitimu wa kike kwa asilimia 49 katika
fani mbalimbali katika chuo hicho ni jambo la kujivunia na kuwapongeza
wakufunzi wa chuo hicho kwa kazi nzuri wanayoifanya ya utoaji wa elimu
bora.
Naye
kaimu mkuu wa Chuo hicho Bw. Athman Ahmad amewapongeza wahitimu hao
waliotunukiwa vyeti katika fani 30 na kuwataka kutumia ipasvyo elimu
waliyoipata kwa manufaa ya taifa kwa kufanya kazi kwa bidii na kuepuka
tama ya kutaka kupata utajiri kwa muda mfupi pindi wanapofanikiwa
kujiajiri au kuajiriwa.
“Nawaomba
muwe wavumilivu na mjiepushe na vitendo vya kihalifu na kutaka kupata
utajiri kwa kipindi kifupi, najua ninyi ni vijana na mnatamani vitu
vingi kwa wakati mmoja cha msingi mfanye kazi kwa bidii, uaminifu na
kuepuka tamaa zinazoweza kuwafanya muingie katika vitendo viovu”
amesema.
Bw.
Ahmad amesema licha ya chuo hicho kukabiliwa na changamoto ya udogo wa
eneo na uchakavu wa miundombinu pia kina kabiriwa na uhaba wa walimu 20
kuongezea idadi ya 80 waliopo sasa na tayari juhudi mbalimbali
zinaendelea kufanyika ili kuboresha huduma za elimu chuoni hapo na
kuondoa tatizo la uhaba wa madarasa na walimu.
Amesema
chuo hicho kina muda mrefu tangu mwaka 1965 na tayari majengo yake
hayana uwezo wa kuchukua wanafunzi wengi kutokana na idadi kubwa ya
wanafunzi na mwamko mkubwa wa watanzania katika masuala ya elimu jambo
linalowafanya kulazimika kukodi madarasa nje ya chuo.
“Chuo
kilipoanzishwa mwaka 1965 kilikua na wanafunzi 30 na leo hii kwa eneo
la Dar es salaam tuna wanafunzi takribani 9000 hili ni jambo
linalohitaji uboreshaji wa miundombinu na uongezaji wa majengo mapya ili
kukabiliana na changamoto hiyo” amesema Bw. Ahamad .
Kaimu
mkuu wa chuo hicho amefafanua kuwa hivi sasa chuo kina mkakati wa
kuongeza mafunzo ya shahada ya uzamili na kuongeza majengo ya madarasa
katika kampasi zote 3 za Dar es salaam, Dodoma na Mwanza.
“Jambo
hili tuko makini nalo na sasa kazi ya uchoraji wa michoro na juhudi za
kutafuta fedha wakiwemo wafadhiri zinaendelea kufanyika ili kuweza
kukamilisha mipango hiyo.
Mahafali
hayo ya 47 yaliyofanyika jana jioni katika viwanja vya Mnazi mmoja
jijini Dar es salaam yalihudhuriwa na wananchi kutoka maeneo mbalimbali
na viongozi wa Bodi ya Chuo hicho wakiongozwa na Prof. Mathew Luhanga
kutoka Chuo kikuu cha Uhandisi na Teknolojia cha Chuo kikuu cha Dar es
salaa na yatafuatiwa na mahafali mengine katika kampasi ya Dodoma
tarehe 1 na tarehe 8 mwezi Desemba katika kampasi ya Chuo cha Elimu ya
Biashara Mwanza .
No comments:
Post a Comment