Hapa baadhi ya waislamu walioamua liwalo naliwe na kuamua kuwatunishia msuli polisi na kusema pigeni mpendavyo hatoki mtu.
Askari wa jeshi la Polisi kikosi cha kutuliza ghasia wakiwadhibiti vijana waliokuwa wakileta vurugu eneo la mbagala kufuatia kijana mmoja anaesemekana anasoma kidato cha kwanza kukojolea mkojo Quraan na kusababisha hasira kwa waislamu hassa vijana ambao walitapakaa mitaani na kuanza kuleta vurumai. |
Vijana waliosambaa mitaani na kuamsha vurugu kubwa kwenye eneo hilo la Mbagala Kizuiani. |
Waisilamu waliotoka msikitini kwenye swala ya Ijumaa walikumbana na kimbembe cha kamatakamata hatakama hawakuwemo kwenye sakata hilo, alama ni kanzu na sijda |
Barabara zilikua zikiharibiwa kwa moto ulikuwa ukiwashwa na waisilamu hao wenye hasira. |
Maji ya kuwasha yalikuwepo ingawa hayakuweza kuzuia vurugu hizo. |
Askari na watuhumiwa wakivuka pamoja kwenye mtaro wa maji taka. |
Watuhumiwa wavurugu hizo wakipandishwa kwenye gari la polisi. Picha na Mtaa kwa Mtaa Blog
Baadhi ya vizuizi vilivyowekwa na waislam eneo la Mbagala Kizuiani
wakati wa maandamano yaliyofanyika jijini Dar es Salaam leo kupinga
kitabu kitakatifu cha Koran kufanyiwa dhihaka na mtoto Emmanuel Josephat
ambaye aliitemea mate.
Polisi wakiwa katika kuhakikisha hali ya usalama inaimarishwa katika eneo la Mbagala leo
Mmoja wa waandamanaji akiwa amekamatwana askari wa Kikosi cha Kutuliza Ghasia (FFU)
Baadhi ya magari yaliyoharibika katika maandamano ya waislam leo
HAMISI
SALUM BABA MZAZI WA KIJANA AMBAYE MSAAFU WAKE ULIFANYIWA DHIHAKA NA
EMMANUEL JOSEPHAT NA KUZUA MAANDAMANO MAKUBWA YALIYOFANYWA NA WAAISLAMU
JIJINI DAR LEO.Picha na Happy Mnale
DAR ES SALAAM, Tanzania
VURUGU kubwa zimezuka baada ya mtoto Emanuel Josephat(14)’
kukojolea kitabu cha Quraan cha dini ya kiislam limeingia katika hatua nyingine
baada ya waamini wa dini ya kiisilam kukusanyika wakishinikiza kuachiwa kwa mtoto
huyo ili wamuue.
Waamini hao wanaokadiriwa kufikia idadi ya 3000 baada ya
kutawanywa na Polisi waliingia mitaani na kuchoma kanisa la Kiinjili la
Kilutheri Tanzania(KKKT), Mbagala Zakhem, Kuharibu Kanisa la Anglican,kuvunja
vioo katika kanisa la Wasabato, huku kanisa la Tanzania Assembly of God(TAG),
Mbagala Kizuiani wakilichoma moto na kuchukua vifaa vya muziki na kuviunguza
hadharani.
Vurugu hizo zilizotokea jana jijini Dar es Salaam, majira ya saa
5 asubuhi ambapo waislamu hao walivamia kituo cha polisi Maturubai,Mbagala
Kizuiani.
Vurugu hizo ambazo zimesababisha gari za polisi namba T142
AVV,PT 0966 na T 325 BQP,basi la uda na gari la waandishi wa habari kutoka
Clouds zikiharibiwa kwa mawe na waandamanaji hao.
Awali waamini hao walikusanyika katika kituo hicho cha polisi
wakimtaka mtoto huyo ambaye alikuwa chini ya ulinzi aachiwe na Polisi
walipogoma kufanya hivyo ndipo vurugu hizo zilipoanza.
Kikosi cha kutuliza ghasia kilionekana kuzidiwa nguvu na watu
hao ambao walikuwa wakiwatawanya kutoka eneo moja wanakimbilia eneo lingine na
kuleta madhara mbalimbali ikiwa ni pamoja na kufunga barabara.
Hatahivyo baada ya viongozi wa dini hiyo kufika wakiwa wameambatana
na Sheikh wa Wilaya ya Temeke, Sheikh wa Taasisi na Jumuiya za Waislamu kukaa
kikao na kamanda wa Polisi Wilaya ya Temeke, David Misime, walifikia muafaka wa
kuwaita waislamu hao na kuwatuliza lakini hali iliendelea kuwa si shwari kwani
baada ya viongozi hao kuona waandamanaji hao wakikamatwa na kupigwa walikuja
juu na kutishia kuondoka.
“Ndio nini sasa sisi tupo hapa kwa kuleta suluhu lakini ili
waislamu watulie lakini mnawapiga mbele yetu ndio nini sasa
|
No comments:
Post a Comment