MNADHIMU WA JWTZ AAPISHWA NA DR. JAKAYA KIKWETE - Wazalendo 25 Blog

Habari Mpya

Glory to Story.


Post Top Ad


27 Sept 2012

MNADHIMU WA JWTZ AAPISHWA NA DR. JAKAYA KIKWETE


Rais Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. Jakaya Kikwete akimwapisha Luteni Jenerali Samuel Albert Ndomba (kulia) kuwa Mnadhimu Mkuu wa Jeshi la Ulinzi la Wananchi wa Tanzania (JWTZ) katika viwanja vya Ikulu leo jijini Dar es salaam. Meja Jenerali Ndomba anachukua nafasi iliyoachwa wazi na Luteni Jenerali Abdulrahaman Shimbo aliyestaafu utumishi jeshini kwa Umri.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na Amiri Jeshi Mkuu wa Majeshi ya Ulinzi na Usalama Dkt. Jakaya Kikwete akimwapisha Meja Jenerali Raphael Mugoya Muhuga (kulia) kuwa Mkuu wa Jeshi la Kujenga Taifa (JKT) leo Ikulu jijini Dar es salaam.
Rais Dkt. Jakaya Kikwete (katikati) akiwa katika picha ya pamoja na Mkuu wa Majeshi ya Ulinzi nchini Jenerali Devis Mwamunyange (kushoto) na maofisa wa Jeshi Luteni Jenerali Samuel Ndomba, Mnadhimu Mkuu wa JWTZ (wa tatu kutoka kushoto) na Meja Jenerali Raphael Mugoya Muhuga mkuu wa JKT walioapishwa leo Ikulu jijini Dar es salaam.
Rais Jakaya Kikwete akiwa katika picha ya pamoja na Viongozi wa Wizara ya Ulinzi na Maofisa wa JWTZ na Jeshi la Kujenga Taifa. 
Mkuu wa Majeshi ya Ulinzi na Usalama Jenerali Devis Mwamunyange (kushoto) akimweleza jambo Rais Dkt. Jakaya Kikwete (kulia) katika viwanja vya Ikulu jijini Dar es salaam.Wengine ni Mkuu wa Mkoa wa Dar es salaam Saidi Meck Sadiki (katikati).
Rais Dkt. Jakaya Kikwete akiwa na Waziri Mkuu Mizengo Pinda (kulia) akiwaeleza jambo viongozi wa Jeshi la Polisi nchini Inspekta Jenerali Saidi Mwema (wa pili kulia) na Kamishina wa Oparesheni wa Jeshi la Polisi, Paul Chagonja . Kulia ni Mkuu wa Majeshi Jenerali Devis Mwamunyange.

No comments:

Post a Comment

Post Top Ad