ADAM MCHOMVU ATOA SHAVU KWA DJ MDOGO NA MWENYE KIPAJI CHA AJABU - Wazalendo 25 Blog

Glory to Story.

Habari Mpya

PRINTING / GRAPHICS / DESIGN : 0784 643 633

Tuesday, 3 July 2012

ADAM MCHOMVU ATOA SHAVU KWA DJ MDOGO NA MWENYE KIPAJI CHA AJABU


Huyu ndiye Dj Calvy aliyeipagawisha crew ya XXL ya Clouds Fm mjini Arusha.
 Huyu ndiye Dj Calvy aliyewapagawisha crew ya XXL ya Clouds Fm mjini Arusha katika studio za Clouds FM tawi la Arusha.B12, Adam Mchomvu na Ncha kali wakiwa katika kipindi cha redio kilichokuwa kinahusiana na mashindano  ya kuwasaka wasanii wa Fiesta watakaoenda Dar es salaam kuchuana na washindi kutoka mikoani, kilibamba sana baada ya Adam kumpatia nafasi Dj mdogo mwenye umri wa miaka 16 kusimama katika mashine na kuwaacha midomo wazi mastaa hao wa XXL.

Dj Calvy alipewa kugonga ngoma 4 tu, jamaa wakagundua kipaji chake na kutoa tamko la kumpatia ofa ya kumlipia usafiri wa kwenda na kurudi (Dar es Salaam) na huduma zote siku ya BIRTHDAY PARTY yake,na pia agonge ngoma  ndani ya kipindi cha XXL cha Clouds Fm jijini Dar es salaam.

DJ ALI (CLOUDS FM ARUSHA)- Huyu ndiye aliye tengeneza kipaji cha Dj Calvy hadi leo kimeonekana katika crew ya XXL ya Clouds Fm ya Dar. DJ ALI ambae pia ndie kiongozi wa FURAHIA DJ kutoka Arusha amekuwa ni msaada mkubwa kwa ma DJ wengi wanaochipukia mjini Arusha.
MACHOTA (kushoto,na mmiliki wa blog ya ASILI YETU) akiwa na DJ CALVY baada ya mida ya kazi  A- City.

No comments:

Post a Comment