Mhe. Edward Ngoyai Lowassa atembelea ubalozi wa Tanzania Washington DC - Wazalendo 25 Blog

Glory to Story.

Habari Mpya

PRINTING / GRAPHICS / DESIGN : 0784 643 633

Wednesday, 4 July 2012

Mhe. Edward Ngoyai Lowassa atembelea ubalozi wa Tanzania Washington DC

  Wajumbe wa Kamati ya Bunge ya Mambo ya Nje, Ulinzi na Usalama wameanza ziara ya siku mbili Washington DC, kuanzia tarehe 2 - 4 Julai 2012. Pichani, Mwenyekiti wa Kamati ya Bunge ya Mambo ya Nje, Ulinzi na Usalama Mhe. Edward Lowassa (Mb.) akiweka saini kitabu cha wageni mara baada ya kuwasili kwenye ubalozi wa Tanzania Washington DC.
 Mwenyekiti wa Kamati ya Bunge ya Mambo ya Nje, Ulinzi na Usalama Mhe. Edward Lowassa (Mb.)akifuatilia taarifa kutoka Ubalozi wa Tanzania Moscow, kutoka kwa mjumbe wa kamati hiyo Mhe. Vita Kawawa aliyejumuika na msafara huo akitokea  Moscow.
  Kaimu Balozi wa Tanzania nchini Marekani Mhe. Lilly Munanka akipokea zawadi kutoka kwa Mwenyekiti wa Kamati ya Bunge ya Mambo ya Nje, Ulinzi na Usalama Mhe. Edward Lowassa (Mb.) kwenye ofisi za ubalozi

No comments:

Post a Comment