MWENGE WA UHURU WAWASILI JIJINI DAR ES SALAAM LEO, MIRADI YENYE THAMANI YA SH. BILIONI 7 KUZINDULIWA - Wazalendo 25 Blog

Glory to Story.

Habari Mpya

PRINTING / GRAPHICS / DESIGN : 0784 643 633

Monday, 25 June 2012

MWENGE WA UHURU WAWASILI JIJINI DAR ES SALAAM LEO, MIRADI YENYE THAMANI YA SH. BILIONI 7 KUZINDULIWA

  Askari kutoka jeshi la Polisi wakiimarisha ulinzi wakati wa sherehe za mapokezi ya Mwenge wa Uhuru leo jijini Dar es Salaam.
 Mkuu wa wilaya ya Temeke Bi. Sophia Mjema akiahidi mbele ya mkuu wa mkoa wa Dar es Salaam Saidi Meck Sadik kuupokea Mwenge wa Uhuru na kuukimbiza katika maeneo mbalimbali ya wilaya hiyo ambapo miradi 11 itafunguliwa na kuwekewa mawe ya msingi.
Mkuu wa mkoa wa Dar es  Salam Saidi Meck Sadik (kulia) akipokea mwenge wa Uhuru kutoka kwa mmoja wa wakimbiza Mwenge wa Uhuru Kitaifa Bi. Tatu Saidi Mussa leo jijini Dar es Salaam . Mwenge wa Uhuru umewasili  jijini  Dar es Salaam ukitokea Mkoa wa Kusini Pemba.
 Wakimbiza Mwenge kitaifa wakiongozwa na kiongozi wa mbio za Mwenge Capt. Ernest Mwanossa (wa kwanza mbele)  wakianza safari kuelekea maeneo mbalimbali ya wilaya ya Temeke leo jijini Dar es Salaam.
 
 Vijana wa halaiki kutoka wilaya ya Temeke wakiimba wimbo maalum wa Mwenge wakati wa mapokezi leo jijini Dar es Salaam.
Baadhi ya wafanyakazi na wananchi wa mkoa wa Dar es Salaam waliojitokeza kuupokea Mwenge wa Uhuru katika uwanja wa ndege wa Kimataifa wa Dar es salaam leo.  
Picha na Aron Msigwa - MAELEZO

No comments:

Post a Comment