KAMPUNI YA BIA YA SERENGETI YAWAPA MABLOGGER SEMINA YA UENDESHAJI WA MITANDAO NA MAADILI KATIKA KUPASHA HABARI ZA MASOKO. - Wazalendo 25 Blog

Glory to Story.

Habari Mpya

PRINTING / GRAPHICS / DESIGN : 0784 643 633

Thursday, 17 May 2012

KAMPUNI YA BIA YA SERENGETI YAWAPA MABLOGGER SEMINA YA UENDESHAJI WA MITANDAO NA MAADILI KATIKA KUPASHA HABARI ZA MASOKO.



 Mkurugenzi wa mtandao wa www.fullshangweblog.com akipokea cheti chake kutoka kwa Ephraim Mafuru Mkurugenzi wa Masoko wa kampuni ya bia ya Serengeti (SBL) mara baada ya kumalizika kwa semina ya Mablogger kuhusu usimamizi na maadili ya upashaji wa habari na masoko katika  uendeleshaji wa blogu na mitandao mingine, iliyofanyika leo kwenye makao makuu ya kampuni hiyo yaliyoko Oysterbay jijini Dar es salaam, katikati ni mkurugenzi wa mawasiliano wa kampuni hiyo Teddy Mapunda
 Mkurugenzi wa Fullshangweblog Bw. John Bukuku ,kushoto akizungumza na mkurugenzi wa Blog ya 8020fashion,Bi Shamimu Mwasha  mara baada ya semina hiyo, kulia ni Mkurugenzi wa blogu ya Father Kidevu.
Mkurugenzi wa blog ya 8020fashion,Bi. Shamimu Mwasha akipokea cheti chake kutoka kwa Bw. Ephraim Mafuru Mkurugenzi wa Masoko wa kampuni ya bia ya Serengeti (SBL) katikati ni mkurugenzi wa mawasiliano wa kampuni hiyo Bi. Teddy Mapunda.
 Bw. Josephat Lukaza wa LJ Media ,akipokea cheti chake kutoka kwa Bw. Ephraim Mafuru ,Mkurugenzi wa Masoko wa kampuni ya bia ya Serengeti (SBL), katikati ni Bi. Teddy Mapunda Mkurugenzi wa Mawasiliano (SBL) kulia ni David Shayo wa (SBL)
Bw. Mroki Mroki  kutoka blogu ya Father Kidevu blog, kushoto akipokea cheti chake.
 Mwendeshaji wa Blogu ya Mtaa kwa Mtaa blog,Bw. Othman Michuzi kushoto akipokea cheti chake.
 Mkurugenzi wa Blogu ya Jiachie blog, Bw. Ahmed Michuzi kushoto akipokea cheti chake.
 Mkurugenzi wa kampuni ya R&R Caroline Gul kushoto  akipokea cheti chake.
 Mkurugenzi wa mawasiliano wa kampuni ya bia ya Serengeti Teddy Mapunda akifafanua jambo katika semina ya uendeshaji wa mitandao na maadili ya upashaji wa habari za masoko katika blogu na mitandao mingine.

No comments:

Post a Comment