Siku za kumkamata Bosco Ntaganda zinakaribia - Wazalendo 25 Blog

Glory to Story.

Habari Mpya

PRINTING / GRAPHICS / DESIGN : 0784 643 633


PRINTING / GRAPHICS / DESIGN : 0676 643 633

Thursday, 17 May 2012

Siku za kumkamata Bosco Ntaganda zinakaribia



Bosco Ntaganda na waasi wake

Mwendesha mashtaka mkuu katika mahakama ya kimataifa ya ICC, amesema kuwa ana matumaini Generali Ntaganda atakamatwa katika muda wa wiki chache tu.
Ntaganda anasakwa na mahakama hiyo, kwa tuhuma za uhalifu dhidi ya binadamu.
Luis Moreno-Ocampo ameiambia BBC kuwa serikali za DR Congo na Rwanda sasa zinaamini kuwa Generali Ntaganda anapaswa kukamatwa na kwamba hali yake sasa ni ya wasiwasi.
Awali, Umoja wa mataifa ulisema kuwa mapigano nchini DRC yamewatorosha maelfu ya raia kukimbilia usalama wao katika nchi jirani.
Mkuu wa shirika la kuwahudumia wakimbizi la umoja huo, Antonio Guterres, alisema kwamba kukithiri kwa mapigano kati ya jeshi na waasi, waliotoroka jeshi na ambao ni watiifu kwa Generali Ntaganda,yamesababisha idadi kubwa ya wakimbizi wanaoomba msaaada katika nchi jirani.
Takriban wakimbizi 30,000 kutoka Congo, wameingia nchini Uganda kutoroka mapigano mapya yaliyozuka tarehe 10 mwezi Mei. Maafisa wa UNHCR wamewanukuu maafisa wa Uganda wakisema raia 8,000 wa Congo wamesajiliwa nchini Rwanda tangu tarehe 27 mwezi Aprili.
Bwana Moreno-Ocampo alisema kuwa sasa kuna uelewa unaostahili kati ya nchi hizo mbili, kuhusu uhalifu uliotendwa na Generali Ntaganda, anayejulikana kama "The Terminator" kuliko mara ya kwanza ambapo mahakama ya ICC ilitoa kibali cha kumkamata Ntaganda mwaka 2006, kwa tuhuma za kuwasajili watoto jeshini.
Siku mbili zilizopita bwana Moreno-Ocampo alisema ananua kutoa kibali cha kumkamata kiongozi mwingine wa waasi, Sylvestre Mudacumura na kutaka kumuongezea mashtaka Generali Ntaganda.
Baadhi ya maafisa wa Congo, wameshtumu serikali ya Rwanda kwa kumuunga mkono Generali Ntaganda, ambaye alipigana na waasi wa kabila la Tutsis, na ambao sasa ndio wanatawala nchi hiyo.

No comments:

Post a Comment