Aliyekuwa Mbunge wa Arusha Mjini Bw. Godbless Lema kwa tiketi ya CHADEMA akitoka mahakamani mara baada ya kuvuliwa ubunge na mahakama ya hapa Arusha,pembeni ni Mbunge mpya wa Arumeru Mashariki Bw. Joshua Nassari na wadau wengine wa chama cha CHADEMA.
MAHAKAMA Kuu Kanda ya arusha leo imemvua Ubunge aliyekuwa Mbunge wa jimbo la Arusha mjini Godbless Lema kwa tiketi ya CHADEMA.
Taarifa kutoka jijini Arusha zinasema uamuzi huo umefikiwa leo asubuhi Aprili 5, 2012 mbele ya Jaji Mfawidhi wa Kanda ya Sumbawanga, Gabriel Rwakibarila katika hukumu ya kesi ya kupinga matokeo ya Ubunge Jimbo la Arusha hilo yaliyo wasilishwa nawanachama watatu wa CCM waliotaka Mahakama Kuu Kanda ya Arusha kutengua ushindi wa Mbunge huyo.
Wana CCM hao waliofungua kesi hiyo ni pamoja na Mussa Mkanga (55), Happy Kivuyo (49) na Agnes Mollel (44).
Lema katika Uchaguzi huo alikuwa akichuana vikali na Mgombea wa CCM, Dk. Batilda Salha Buriani ambaye kwa sasa ni Balozi wa Tanzania nchini Kenya.
Wana CCM hao waliofungua kesi hiyo ni pamoja na Mussa Mkanga (55), Happy Kivuyo (49) na Agnes Mollel (44).
Lema katika Uchaguzi huo alikuwa akichuana vikali na Mgombea wa CCM, Dk. Batilda Salha Buriani ambaye kwa sasa ni Balozi wa Tanzania nchini Kenya.
Kuvuliwa Ubunge kwa Lema, kuna kuja siku chache wakati bado chama hicho kipo katika shamra shamra za ushindi wa Ubunge jimbo la Arumeru Mashariki mkoani humu.
Pia habari za ndani ya Chama cha Chadema zinasema kuwa tayari Chama hicho kilisha soma alama za nyakati mapema katika kesi hiyo miezi kadhaa nyuma na kujipanga endapo mbunge huyo atavuliwa wadhifa wake nani kimsimamishe kutetea kiti hicho.
Habari hizo zinadai kuwa Chadema kimepanga kumsimamisha Katibu Mkuu wa Chama hicho na Mgombea Urais wa 2010, Dk. Wilbroad Silaa kutetea kiti hicho.
Wanachama hao wanadai kuwa taratibu za maadili ya uchaguzi zilikiukwa wa kuwa mshindi alitumia lugha za kashfa, matusi na kejeli katika mikutano ya kampeni aliyofanya jimboni Arusha.
Katika kesi hiyo wadai walileta mashahidi 14 kwenda kutoa ushahidi wao katika mahakama hiyo nawadaiwa walifanikiwa kuwaleta mashahidi 5 kujitetea.
No comments:
Post a Comment