WANAHABARI WASHINDANA KUONJA LADHA YA BIA ZA TBL ARUSHA - Wazalendo 25 Blog

Glory to Story.

Habari Mpya

PRINTING / GRAPHICS / DESIGN : 0784 643 633

Tuesday, 13 March 2012

WANAHABARI WASHINDANA KUONJA LADHA YA BIA ZA TBL ARUSHA


Ofisa Uhusiano na Mawasiliano wa Kampuni ya Bia Tanzania (TBL), Edithi Mushi (kushoto), akimkabidhi zawadi ya bia Mwenyekiti wa Chama cha Waandishi wa Habari mkoani wa Arusha (APC), Graud Gwandu baada ya kushika nafasi ya pili katika shindano la kutambua radha za bia za  aina mbalimbali zinazozalishwa na TBL, katika shindano lililokutanisha wanahabari wa mkoa huo mwishoni mwa wiki.
Ofisa Uhusiano na Mawasiliano wa Kampuni ya Bia Tanzania (TBL), Edith Mushi  (kushoto) akimkabidhi zawadi ya katoni tatu za bia mwandishi wa gazeti la Majira, Pamela  Mollel ambaye alishinda shindano la kutambua radha za aina mbalimbali za bia zinazozalishwa na kampuni hiyo. Shindano hilo lilikutanisha wanahabari wa Mkoa wa Arusha mwishoni mwa wiki.
 Meneja wa Kanda ya Kaskazini Mashariki wa Kampuni ya Bia Tanzania (TBL), Kasilo Msangi akizungumza na waandishi wa habari katika kiwanda cha TBL mkoani Arusha mwishoni mwa wiki, kuelezea mafanikio makubwa ya kampuni hiyo kwa kanda hiyo.
Baadhi ya waandishi wa habari Mkoa wa Arusha, wakitembelea kiwanda cha Kampuni ya Bia Tanzania (TBL) mkoani Arusha, mwishoni mwa wiki.

No comments:

Post a Comment