RAISI Dr. JAKAYA KIKWETE AFUNGUA WARSHA YA MIKAKATI YA KUONDOA UMASKINI JIJINI DAR - Wazalendo 25 Blog

Habari Mpya

Glory to Story.


Post Top Ad


29 Mar 2012

RAISI Dr. JAKAYA KIKWETE AFUNGUA WARSHA YA MIKAKATI YA KUONDOA UMASKINI JIJINI DAR



Rais Jakaya Mrisho Kikwete akifungua warsha ya siku mbili ya mikakati ya kiuchumi ya kuondoa umaskini iliyoandaliwa na REPOA katika hoteli ya White Sands jijini Dar es salaam.
(PICHA NA IKULU)
Rais Dkt Jakaya Mrisho Kikwete akipongezwa kwa hotuba nzuri ya ufunguzi na  Mwenyekiti wa Bodi ya Wakurugenzi wa REPOA Profesa Esther Mwaikambo na kulia ni Mkurugenzi Mtendaji wa REPOA Profesa Samuel Wangwe
 Rais Dkt Jakaya Mrisho Kikwete akimsikiliza  Katibu Mtendaji a Tume ya Mipango Dkt Phillip Mpango  akitoa mada ya ufunguzi wa warsha hiyo ya siku mbili ya REPOA. Wengine toka shoto  Mwenyekiti wa Bodi ya Wakurugenzi wa REPOA Profesa Esther Mwaikambo na kulia ni Mkurugenzi Mtendaji wa REPOA Profesa Samuel Wangwe na Balozi wa Uholanzi nchini Dkt Ad Koekkoek.

Rais Dkt Jakaya Mrisho Kikwete akimpongeza Katibu Mtendaji a Tume ya Mipango Dkt Phillip Mpango  kwa mada nzuri. Kati yao ni  Mwenyekiti wa Bodi ya Wakurugenzi wa REPOA Profesa Esther Mwaikambo na kulia ni Mkurugenzi Mtendaji wa REPOA Profesa Samuel Wangwe na Balozi wa Uholanzi nchini Dkt Ad Koekkoek.
Profesa Do Duc Dinh toka Vietnam akitoa mada ya jinsi nchi yake ilivyofanikiwa kuondoa umaskini warsha ya siku mbili ya utafiti juu ya mageuzi ya kuondoa umaskini nchini.

Rais Dkt Jakaya Mrisho Kikwete akiongea na Profesa Ibrahim Lipumba baada ya picha ya pamoja na washiriki wa warsha ya siku mbili ya utafiti juu ya mageuzi ya kuondoa umaskini.
Rais Dkt Jakaya Mrisho Kikwete akiongea na Mwenyekiti wa Bodi ya Wakurugenzi wa REPOA Profesa Esther Mwaikambo, Mkurugenzi Mtendaji wa REPOA Profesa Samuel Wangwe, Balozi wa Uholanzi nchini Dkt Ad Koekkoek, Katibu Mtendaji a Tume ya Mipango Dkt Phillip Mpango na Mkuu wa Mkoa wa Dar es salaam Mh Saidi Meck Sadick muda mfupi kabla ya kuondoka hoteli ya White Sands Hotel alikofungua warsha ya siku mbili ya Utafiti.

No comments:

Post a Comment

Post Top Ad