MAKAMU WA RAIS DKT. BILAL ATEMBELEA MASHAMBA YA MPUNGA YA KOROGWE, AWEKA JIWE LA MSINGI JENGO LA UKUMBI NA OFISI YA HALMASHAURI YA KOROGWE - Wazalendo 25 Blog

Glory to Story.

Habari Mpya

PRINTING / GRAPHICS / DESIGN : 0784 643 633

Friday, 27 January 2012

MAKAMU WA RAIS DKT. BILAL ATEMBELEA MASHAMBA YA MPUNGA YA KOROGWE, AWEKA JIWE LA MSINGI JENGO LA UKUMBI NA OFISI YA HALMASHAURI YA KOROGWE

Makamu Wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akisalimiana na Madiwani wa Kata za Wilayani Korogwe, alipowasili eneo hilo kwa ajili ya kuweka Jiwe la Msingi katika Jengo la Ukumbi na Ofisi ya Halmashauri ya Wilaya ya Korogwe, wakati akiwa katika ziara yake ya Wilaya ya Korogwe mkoa wa Tanga.
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akiweka Jiwe la Msingi katika jengo jipya la Ukumbi na Ofisi ya Halmashauri ya Wilaya ya Korogwe, wakati alipokuwa katika ziara yake ya kukagua miradi ya maendeleo ya Wilaya ya Korogwe mkoa wa Tanga.
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal na Viongozi wa Wilaya ya Korogwe, wakikagua jengo la Ukumbi na Ofisi ya Halmashauri ya Korogwe baada ya kuweka jiwe la Msingi katika jengo hilo alipokuwa kwenye ziara yake ya kukagua miradi ya maendeleo ya wilaya hiyo.
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akisikiliza maelezo kutoka kwa mmoja wa wakulima wa Mpunga kuhusu kilimo hicho cha umwagiliaji wakati alipotembelea na kukagua mashamba ya Skim Mamlaka ya mji wa Mombo.
Makamu wa Rais wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohamed Gharib Bilal, akikagua mitaro ya maji yanayotumika kumwagilia mashamba ya mpunga ya Skim, mji wa Mombo, wakati akiwa katika ziara yake ya kukagua miradi ya maendeleo ya Wilaya ya Korogwe mkoa wa Tanga.
Picha na Muhidin Sufiani-OMR

No comments:

Post a Comment