Kamati ya bunge ya maadili yafanya ziara Clouds Media Group mikocheni jijini Dar. - Wazalendo 25 Blog

Glory to Story.

Habari Mpya

PRINTING / GRAPHICS / DESIGN : 0784 643 633

Friday, 27 January 2012

Kamati ya bunge ya maadili yafanya ziara Clouds Media Group mikocheni jijini Dar.

Mwenyekiti ya Kamati ya Bunge ya Maendeleo ya Jamii,ambaye pia ni Mbunge wa jimbo la Peramiho,Mh Jenista Mhagama akizungumza jambo mbele ya kamati hiyo (haipo pichani) pamoja na uongozi wa Clouds Media Group mapema leo,Mikocheni jijini Dar,ambapo kamati hiyo imefanya ziara ndani ya kampuni hiyo na kujionea mambo mbalimbali yanayofanywa na kampuni hiyo.Aidha Mh. Mhagama ameisifu na kuipongeza kwa kiasi kikubwa kampuni hiyo kwa utendaji wao mzuri wa kazi na pia kaitoa nafasi kubwa ya ajira kwa vijana.
Akisalimiana na Mkurugenzi wa Prime Time Promotions Ltd,Jayna Kusaga ambao ndio waandaaji bingwa wa matamasha mbalimbali hapa nchini,ambapo kamati ya bunge ya Maendeleo ya jamii pia ilizitembelea ofisi hizo zilizopo ndani ya jengo la Clouds Media Group.
Mbunge wa jimbo la Mbinga Magharibi,Mh John Komba akieleza kuwa yeye ndiye muanzilishi wa kipindi cha Leo Tena,tangu enzi za Marehemu Amina Chifupa ,ambacho kinaendelea mpaka sasa,Mh. Komba alikuwa akizungumza hayo ndani ya kipindi cha Leo Tena wakati kamati hiyo ilipotinga ndani ya studio hizo na kujionea mitambo mbalimbali ya kisasa inavyofanya kazi.Pichani kushoto ni Mtangazaji wa kipindi cha Leo Tena,Dina Marios.
Akiwapongeza watangazaji wa kipindi cha Leo Tena,shoto ni Mtangazaji wa kipindi hicho Bi. Gea Habib a.k.a Mama wa heka heka na kulia ni mtayarishaji wa baadhi ya vipindi vya Clouds Fm,Simalenga
Mh. Jenista Mhagama akizungumza jambo ndani ya studio za clouds fm akiwa sambamba na kamati yake huku kipindi cha Leo Tena kikiendelea.
Mbunge wa jimbo la Mbinga Magharibi,Mh John Komba akieleza kuwa yeye ndiye muanzilishi wa kipindi cha Leo Tena,tangu enzi za Marehemu Amina Chifupa ,ambacho kinaendelea mpaka sasa,Mh Komba alikuwa akizungumza hayo ndani ya kipindi cha Leo Tena wakati kamati hiyo ilipotinga ndani ya studio hizo na kujionea mitambo mbalimbali ya kisasa inavyofanya kazi.Pichani shoto ni Mtangazaji wa kipindi cha Leo Tena,Dina Marios.
Mkurugenzi Mtendaji wa Clouds Media Group,Bw.Joseph Kusaga (Jo ) akitoa historia fupi ya kampuni hiyo ikiwemo sambamba na utendaji kazi wake na mengineyo mbele ya kamati ya Bunge ya Maendeleo ya Jamii iliyofanya ziara ndani ya kumpuni hiyo na kujifunza/kujionea mambo mbalimbali ya kiutendaji.


Kamati ya Bunge ya Maendeleo ya Jamii, ikiongozwa na Mwenyekiti wake Mh.Jenista Mhagama wakiendelea na majadiliano kuhusu mambo mbali mbali kuhusiana na kampuni ya Clouds Media Group sambamba na baadhi ya viongozi wa juu wa kampuni hiyo.
Mmoja wa mainjinia wa Clouds TV,Mebb Hadhad akifafanua jambo kuhusiana na urushaji wa matangazo ya TV mbele ya kamati hiyo.
Mkurugenzi Mtendaji wa Clouds Media Group,Bw.Joseph Kusaga ( Jo) akiwatambulisha baadhi ya wafanyakazi wa kampuni hiyo mbele ya kamati ya Bunge ya Maendeleo ya Jamii.

No comments:

Post a Comment