Kundi la raia wa Rwanda walionusurika na mauaji ya kimbari limeshutumu hatua ya Shirika la kutetea haki za binadamu kutoa tuzo kwa mmiliki wa Hotel Rwanda kwa kuwasiaida watu wakati wa mauaji hayo.
Paul Rusesabagina, aliyetia for katika filamu ya Hotel Rwanda Hollywood alipewa tuzo na shirika la Lantos Foundation linalotetea haki za binadamu na Usawa.Lakini kundi la Ibuka linasema alitia chumvi jukumu lake la kusaidia wakimbizi kutoka hotelini katika siku mia moja za mauaji mwaka 1994
Mr Rusesabagina kwa sasa anaishi uhamishoni na mkosaoji mkubwa wa serikali.
Ibuka ni kundi lililo karibu na Rais Paul Kagame, ambaye majeshi yake yalimaliza mauaji ya zaidi yaw watu 800,000 watutsi na wahutu wenye msimamo wa wastani walipokamatwa mji mkuu Kigali.
Njia mbadala
Filamu hiyo ya Hotel Rwanda ya mwaka 2004 inaelezea jinsi Bw Rusesabagina, Mhutu wa daraja la kati aliyeoa mtutsi alitumia ushawishi wake na hongo kuwashawishi maafisa wa jeshi kutoroka salama kwa watu wapatao 1,200 walioomba hifahdi katika hotel ya Mille Collines mjini Kigali."Tatizo letu ni kile wanachofanya, ni kwa sababu ya ile filamu Hotel Rwanda – hiyo sio habari ya kweli, " Janvier Forongo, katibu mtendaji wa Ibuka, alisema kuhusu kupewa tuzo kwa Bw Rusesabagina.
Ikiwa Paul Rusesabagina hakuwa na lengo la kuwavuta hisia za kuhusu yale yanayotokea Rwanda leo, hakuna kitu kingetokea”
Katrina Lantos Swett, Lantos Foundation
"Alikuwa akiwatoza pesa wale walionusurika katika ile hotel," alisema.
Katrina Lantos Swett, Rais wa Lantos Foundation, alisema meneja wa zamani wa hotel hiyo amepewa pia tuzo ya ‘kuendelea kuwa jasiri’ kuzungumzia kuhusu ukandamizaji wa kisiasa nchini Rwanda.
"Kutokuwepo kwa demokrasia, kuzuia uhuru wa habari, kuwafunga wapinzani wa kisiasa, hivi ni vyanzo vya wasiwasi na inataka moyo kuyazungumza wakati sasa kuna serikali Rwanda ambayo haichukulii vizuri ukosoaji huo," alikiambia kipindi cha BBC World Today.
Ibuka, na kundi lingine la watu walionusurika limemshutumu pia Bw Rusesabagina kuwa na uhusiano na wapiganaji wa Kihutu walioko DRC na mwendesha mashtaka amemtuhumu kwa kutuma fedha kwa makamanda huko.
Bw Rusesabagina ameiambia BBC kuwa tuhuma hizo ni kujaribu “kubadilisha mwelekeo wa jumuiya ya kimataifa kutoka kwenye ukweli halisi wa matatizo," Rwanda kama vile ukandamizaji wa upinzani.
Washindi waliopita wa tuzo ya Lantos ni pamoja na kiongozi wa kiroho wa Tibet Dalai Lama na manusura wa mauaji Ellie Wiesel.
"Unapokuwa na mtu anayeibuka kama sauti inayopinga utawala, mara nyingi ama wanaowaunga mkono au njia mbadala watajitokeza mbele zaidi kumpinga mtu huyo," alisema Bi Lantos Swett.
"Nimehakikishiwa – namfahamu Paul Rusesabagina, ninaamini kuwa yeye ni mfano kwa wengi wetu, alifanya kile alichotakiwa kufanya siku hadi siku, katika ulimwengu wake mdogo, kujaribu na kuokoa maisha ya watu.”
"Haikutokea wakati filamu hii ilipotoka… ni wakati alipoanza kuzungumza tu ndio ghafla wengi wanauliza na kuja na tuhuma ambazo si za kweli zinaibuliwa."
No comments:
Post a Comment