MWENDELEZO WA MATUKIO YA TAMASHA LA SERENGETI FIESTA LILILOFANYIKA USIKU WA KUAMKIA JPILI LEADERS CLUB. - Wazalendo 25 Blog

Habari Mpya

Glory to Story.


Post Top Ad


2 Aug 2011

MWENDELEZO WA MATUKIO YA TAMASHA LA SERENGETI FIESTA LILILOFANYIKA USIKU WA KUAMKIA JPILI LEADERS CLUB.

Shughuli nzima ya Msimu wa Dhahabu na Serengeti Fiesta ilifungwa na mkali Ludacriss kutoka nchini Marekani, kama unavyomuona katika picha hii akiimbisha mashabiki wake hawapo pichani, wakati aliposhusha burudani kabambe katika viwanja vya Leaders usiku wa kuamkia Jpili jijini Dar es salaam. Oooya Oya oya Starehe Gharamaa!, Oooya Oya oya Starehe Gharamaaaa ni vijana wa Tiptop Connection hawa wakishabulia jukwaa.
Prof Jay au Jay wa Mitulinga kama wanavyomuita mashabiki wake akifanya vitu vyake jukwaani.
Mashabiki wameshachenguka na burudani kama unavyowaona mikono juujuu.
ML Chriss kutoka Choice FM na Christiane Mosha aka Seven mwakilishi wa MTV hapa nchini wakishoo love katika picha.
Ulinzi ulikuwa ni wa kiwango cha hali ya juu kama unavyoona katika picha hii wanausalama wakiwa tayari kabisa kukabiliana na vurugu zozote ambazo zingeweza kutokea.
Binamu MwanaFA akiwakilisha kwa mashabiki wake kama unavyomuona katika picha.
Lina alitisha kwa kivazi chake hebu kicheki mdau.
Juma Nature akicheza na meneja wake jukwaani anayejulikana kama Kiboya mara baada ya kupokea tuzo yake akiwa ni mmoja wa wasanii waliotisha kwa muda mrefu.
Mwanamuziki Diamond akiimba kwa pamoja na Duly Sykes katika tamasha la Serengeti Fiesta usiku wa kuamkia leo.
Wasanii Mdojo na Domokaya walikumbusha enzi zao na wakakamua vilivyo jukwaani.
Kutoka kulia ni Mdau Emilian Rwejuna, Mkurugenzi mtendaji wa SBL Richard Wells, Meneja wa kinywaji cha Serengeti Lager Allan Chonjo na Mkurugenzi wa Masoko SBL Ephraim Mafuru, wakiwa wameshikilia Golden Moments zao za Serengeti Lager
Kutoka kulia ni Ephraim Mafuru Mkurugenzi wa Masoko SBL, Joseph Kusaga Mkurugenzi wa kampuni ya Clouds Entarteiment, Omar kutoka Push Mobale, Caroline Ndungu kutoka SBL na mdau wa blogu Emilian Rwejuna.
Mkurugenzi mtendaji wa SBL Richard Wells akiwa katika picha ya pamoja na Mkurugenziwa Mawasiliano Kampuni hiyo Teddy Mapunda.
Mkurugenzi wa Mawasiliano SBL Teddy Mapunda kushoto akiwa katika picha ya pamoja na Bakari Machumu Mhariri Mkuu wa gazeti The Citizen katikati nia Paul Owere Mwandishi mwandamizi gazeti la The Citizen.
Carol Mkurugenzi wa R&R kushoto akiwa katika picha ya pamoja na Mshiriki wa Project Fame All Stars Peter Msechu wakipata kinywaji cha Serengeti Lager katika tamasha la Serengeti Fiesta jana.
 
Picha na: FULLSHANGWE BLOG

No comments:

Post a Comment

Post Top Ad