Timu ya Yanga ya jijini Dar es salaam leo imefanikiwa kuitoa timu ya St. George ya Ethiopia, baada ya kuiondosha katika mashindano ya Kombe la Kagame Castle Cup kwa penati 5-4 kwenye mchezo wa nusu fainali ,uliofanyika kwenye uwanja wa Taifa jijini Dar es salaam Tanzania leo.
Katika mchezo huo ambao ulikuwa ni wa vuta nikuvute kwa kila upande hakuna timu iliyofanikiwa kuliona lango la mwenzake, hata hivyo ziliongezwa dakika 30 baada ya kipindi cha kawaida cha dakiki 90 kumalizika kwa sare ya 0-0. Kwa maana hiyo Yanga itakutana na watani wao wa jadi timu ya Simba ya Tanzania pia ambayo ilifanikiwa kutinga fainali jana, baada ya kuikung'uta timu ya El Mereck ya Sudan kwa penati 6-5 pia.
Mchezo wa fainali unatarajiwa kuwa mgumu sana hapo jumapili kutokana na timu zote mbili kufahamiana vyema kimchezo, lakini akihojiwa na mtangazaji wa Supersport Thomas Mlambo kocha wa Yanga Sam Timbe, Amesema "Simba imejiandaa vizuri kwani imecheza michezo kadhaa mikubwa na timu zilizoko kwenye viwango vya juu, kama vile TP Mazembe Motema Pembe na zingine ukilinganisha na timu yake ya Yanga". Hata hivyo ameongeza kuwa "muda uliopo unatosha ataangalia mapungufu na kuyarekebisha kwa ajili ya mchezo wa fainali, ambao anaamini utakuwa mzuri na wenye ushindani mkubwa" Amemaliza Sam Timbe.
MWANAMKE MMOJA AFARIKI DUNIA AJALI YA ROLI MBEZI KWA MSUGULI
-
NA EMMANUEL MBATILO, MICHUZI TV
Mwanamke mmoja amefariki dunia baada ya gari aina ya roli lenye namba ya
usajili T696 CLY kuacha njia na kumgonga mwanamke ...
4 hours ago
No comments:
Post a Comment