TANGA YAZIZIMA NA TAMASHA LA SERENGETI FIESTA USIKU WA JANA - Wazalendo 25 Blog

Glory to Story.

Habari Mpya

PRINTING / GRAPHICS / DESIGN : 0784 643 633

Monday, 25 July 2011

TANGA YAZIZIMA NA TAMASHA LA SERENGETI FIESTA USIKU WA JANA

Mwanamuziki Ali Kiba kushoto akiimba na mdogo wake Abdu Kiba kulia, huku mmoja wa wacheza shoo wake akicheza nao, katika tamasha la mwendelezo wa msimu wa Dhahabu na Serengeti Fiesta linalofanyika usiku huu kwenye uwanja wa Mkwakwani Mkoani Tanga, wakati wowote wasanii wakali katika muziki wa bongofleva wataanza kupanda jukwaani.Msanii wa muziki wa bongofleva Bob Junior aka Rais wa Masharobalo akiimba huku wacheza shoo wake wakimpa tafu kwa kunyonga viuno kikamilifu.
MwanaFA akionyesha ujwezo wake mbele ya mashabiki wa mkoa wa Tanga katika tamasha la Serengeti Fiesta lililofanyika katika uwanja wa Mkwakwani Mkoani Tanga, MwanaFA ni mwenyeji wa mkoa wa Tanga.
Mashabiki wakiwa wamechenguka na burudani iliyokuwa ikitolewa na wasanii mbalimbali katika uwanja wa Mkwakwani.
Ni Full Majotroo kwa mashabiki katika uwanja wa Mkwakwani.
Kutoka kulia ni Mkurugenzi wa Clouds Joseph Kusaga, Caroline Ndungu aliyekuwa mkutugenzi wa masoko wa kampuni ya bia ya Serengeti ambaye anarudi Nairobi kwa kazi nyingine ya kampuni ya EABL na Mr John Mkuu wa Usalama kampuni ya SBL wakiwa katika picha ya pamoja.
Mstari wa mbele kutoka kulia ni Wakuvanga kutoka kundi la Orijino Komedi, Joh Makini aka Mwamba wa Kaskazini, Msanii Mpoki kutoka kundi la Orijino Komedi pia na nyuma ni Profesa Jay kulia na Adam Mchomvu wakishoo love.
Profesa Jay kulia akipiga stori na mmoja wa mashabiki wake ambaye alionekanakuwa na shauku kubwa baada ya kukutana na mwanahiphop huyo, anayewashuhudia katikati ni Jeff Msangi anayeendesha mtandao wa BongoCelebrity.
KIjana Juma Mataluma akishambulia jukwaa na wacheza shoo wake.
Beele9 kama kawaida yake amefanikiwa kuwaimbisha mashabiki wake usiku huu.
Mdau wa blog ya Mroki akijipendelea kwa glasi ya bia ya Serengeti Lager huku akiwa ameshikilia Camera yake, kama ishara ya kuonyesha kwamba yuko kikazi zaidi pamoja na kupata kilaji hicho.
Wasanii wa kundi la Makomandoo kutoka THT wakishambulia jukwaa.
Msanii Sheta kushoto na Mwenzake wakichungulia katika kidirisha cha pazia haikufahamika walikuwa wanaagalia nini l;akini ndiyo raha zenyewe za Serengeti Fiesta.
Mkurugenzi wa Clouds Joseph Kusaga akimsikiliza kwa makini mdogo wake Anderw maarufu kama Toperdo, wakati tamasha la Serengeti Fiesta usiku huu kwenye uwanja wa Mkwakwani mjini Tanga.
Wasanii Bekar kulia na Tash wakiim ba katika tamasha hilo.
Msanii Criss Wamalya akmifanya vitu vyake jukwaani katika tamasha la Serengeti Fiesta linaloendelea usiku huu mjini Tanga.
Msanii kutoka kundi la THT Diana akiimba jukwaani usiku huu katika
Nyomi ikiendelea kuongezeka
Mashabiki wa mkoa wa Tanga ni Wastaarabuy kama unavyowaona wakiwa wametulia tuli wakisubiri burudani.
Msanii wa Orijino Komedi Wakuvanga kushoti akiwa katika picha ya pamoja na Mtangazaji wa Clouds Adam Mchomvu.
Mkurugenzi wa Masoko Kampuni ya bia ya Serengeti Breweriers (SBL) Ephraim Balozi Mafuru kushoto, akiwa katika picha ya pamoja na Mkurugenzi wa Mawasiliano wa (SBL) Teddy mapunda, wakifurahia jambo katika tamasha la Msimu wa Dhahabu unaoendelea na Serengeti Fiesta
Kutoka kulia ni Mkurugenzi wa Masoko (SBL) Epharaim Mafuru, Mkurugenzi wa Mawasiliano (SBL) Teddy Mapunda, Meneja Mahusiano ya Jamii (SBL) Nandi Mwiyombela na Mkurugenzi wa Primetime Promotions Ltd Godfrey Kusaga wakishoo Love.
Wakuu wa kampuni ya bia ya Serengeti na wakuu wa kampuni ya Primetime Promotions na wafanyakazi wa Serengeti Breweriers wakiwa katika picha ya pamoja katika tamasha la Serengeti Fiesta linaloendelea usiku huu katika uwanja wa Mkwakwani mjini Tanga.
Huu ndiyo umati uliokwishaingia uwanjani mpaka sasa.
Umati ukisubiri burudani kuanza usiku huu katika uwanja wa Mkwakwani.
Mambo yameanza kunoga katika uwanja wa Mkwakwani mjini Tanga.
 
PICHA ZOTE NA: FULL SHANGWE BLOG

No comments:

Post a Comment