Na Said Mwishehe, Michuzi TV-Karagwe

Aidha, Wasira ameahidi kulifikisha suala hilo kwa Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Innocent Bashungwa alitafute ufumbuzi wa haraka kuhakikisha wageni wote wanazingatia na kufuata utaratibu sahihi wa kuingia na kuishi nchini.
Wasira ameyaleza hayo leo Machi 23, 2025 alipokuwa akizungumza na wanachama wa CCM Wilaya ya Karagwe na Kyerwa mkoani Kagera ambao walimweleza kuwa kuna wageni kutoka nchi jirani wanapora ardhi ya Watanzania katika baadhi ya maeneo ya wilaya hizo.
“Nataka kuwaambia viongozi wetu wa vijiji na vitongoji msiwakaribishe, hatuwazuii kuja kwetu lakini waje kwa kufuata utaratibu. Mkiwaruhusu wakaingia wakajenga nyumba tena za kudumu siku ya kuwatoa itakuwa vita na watasema kuna vita vya wenyewe kwa wenyewe, kumbe kuna vita ya wageni na Watanzania walionyang’anywa ardhi,” ameema.
Amesisitiza kuwa kama kuna jambo gumu duniani ni ardhi, hivyo wananchi wa mipakani wakiruhusu ikaangiliwa itakuja kuleta shida hapo baadaye kwa kuwa ardhi haiongezeki, lakini watu wanaongezeka.
“Kama kuna jambo gumu duniani ni ardhi, mkiruhusu ardhi yenu ikaingiliwa, mnasema kubwa, huku mnazaa namna hii, watu wanaongezeka kwa asilimia tatu kwa mwaka. Wakati nchi inapata uhuru tulikuwa milioni nane lakini leo tuko watu milioni 63, hawa ni watu wengi wanaongezeka.
“Ardhi inabaki ile ile, kwa hiyo msisherehekee jambo hili, sisi tuliwapeni viongozi wa vijiji na vitongoji mamlaka ya kusimamia hakikisheni hawa wageni hawapewi ardhi na hawaingii bila utaratibu.
“Tunawaambia kabisa na hatuna ugomvi kule wanakotoka sisi ni rafiki zetu, lakini na sisi tukitoka hapa Karagwe tukahamia kule watatufukuza tena watatufukuza haraka maana wako wengi na ardhi yao ni ndogo, nchi yao ina watu milioni 12 lakini ukubwa wake ni unazidiwa na Mkoa wa Kagera,” amesema.
No comments:
Post a Comment