Kimataifa : Rais Samia aelekea Rio de Janeiro nchini Brazili kushiriki Mkutano Wakuu wa Nchi na Serikali wa nchi Wanachama wa Kundi la G20 - Wazalendo 25 Blog

Glory to Story.

Habari Mpya

PRINTING / GRAPHICS / DESIGN : 0784 643 633

Saturday, 16 November 2024

Kimataifa : Rais Samia aelekea Rio de Janeiro nchini Brazili kushiriki Mkutano Wakuu wa Nchi na Serikali wa nchi Wanachama wa Kundi la G20


Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan akiagana na Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam Mhe. Albert Chalamila katika Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Julius Nyerere (JNIA) tarehe 16 Novemba, 2024 kabla ya kuelekea Rio de Janeiro nchini Brazil kwa ajili ya kushiriki Mkutano wa Wakuu wa Nchi na Serikali wa nchi Wanachama wa Kundi la G20.  Rais Dkt. Samia amealikwa na Rais wa Brazil Mhe. Luiz Inácio Lula da Silva ambapo pamoja na mambo mengine, atashiriki mijadala inayolenga kuimarisha ushirikiano wa kimataifa katika mapambano dhidi ya njaa na umaskini, kuchochea maendeleo endelevu na matumizi ya nishati mbadala.




 Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan akipanda ndege kuelekea Rio de Janeiro nchini Brazil kwa ajili ya kushiriki Mkutano wa Wakuu wa Nchi na Serikali wa nchi Wanachama wa Kundi la G20.

 Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan akiagana na viongozi mbalimbali katika Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Julius Nyerere (JNIA) tarehe 16 Novemba, 2024 kabla ya kuelekea Rio de Janeiro nchini Brazil kwa ajili ya kushiriki Mkutano wa Wakuu wa Nchi na Serikali wa nchi Wanachama wa Kundi la G20. Rais Dkt. Samia amealikwa na Rais wa Brazil Mhe. Luiz Inácio Lula da Silva ambapo pamoja na mambo mengine, atashiriki mijadala inayolenga kuimarisha ushirikiano wa kimataifa katika mapambano dhidi ya njaa na umaskini, kuchochea maendeleo endelevu na matumizi ya nishati mbadala.

No comments:

Post a Comment