Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Viwanda,Biashara,Kilimo na Mifugo ikiongozwa na Makamu Mwenyekiti wake Mhe. Mariam Ditopile Mzuzuri ikiongozana na Mwenyeji wao Katibu Mkuu wa Wizara ya Viwanda na Biashara Dkt.Hashil Abdallah ikitembelea Kiwanda cha Sukari cha Bagamoyo kwa lengo la kukagua shughuli za sekta binafsi zinazosimamiwa na serikali ili kuhakikisha mwananchi anapata thamani ya kile anachostahiki.
......
WATANZANIA wametakiwa kutambua kuwa serikali ya Rais Dk. Samia Suluhu Hassan haina mpango wa kuviua viwanda vya ndani vinavyozalisha sukari kama wanavyodai baadhi ya watu.
Pia wametakiwa kutambua dhamira ya Rais Dk. Samia ni kukuza viwanda hivyo kuhakikisha uzalishaji wake unaongezeka kuiwezesha nchi kujitosheleza kwa mahitaji ya sukari hususani ya viwandani ndani na nje ya nchi.
Kauli hiyo ilitolewa jana na Makamu Mwenyekiti wa Kamati ya Bunge ya Viwanda, Biashara, Kilimo na Mifugo, Mariam Ditopile alipotembelea kiwanda cha sukari cha Bagamoyo kwa lengo la kukagua shughuli za sekta binafsi zinazosimamiwa na serikali kuhakikiasha mwananchi anapata thamani ya kile anachostahiki kukipata.
“Watanzania puuzeni uzushi wote unaosemwa serikali ya Rais Dk. Samia inataka viwanda vya sukari nchini vife huo sio ukweki, jambo lililotokea lilikuwa la dharura ni lazima serikali iingilie ili kumuokoa mwananchi wa kawaida ambaye ndiye mlaji wa mwisho wa sukari,” alisema.
Alisema Rais Dk. Samia amekuwa akiendelea kuunga mkono juhudi za uwekezaji lengo likiwa kuiwezesha nchi kujitosheleza kwa mahitaji ya sukari hususani ya viwandani.
“Kwa hatua hizi anazozifanya nina uhakika anakwenda kufifikisha nchi ya Tanzania kwenda kuuza sukari nchi jirani na mabara tofauti,” alisema.
Pia alipongeza uwekezaji uliofanywa na kiwanda hicho kwani unachochea ukuaji wa uchumi na ajira hivyo kamati itaendelea kuishauri na kuisimamia serikali kuona kiwanda kinakuwa endelevu na mipango iliyowekwa inakamilika.
Alimpongeza Rais Dk. Samia kwa kuendeleza uwekezaji mkubwa wanaoufanyika kwa kuzishika mkomo sekta binafsi zichangie upatikanaji wa ajira na ukuaji uchumi.
“Kiwanda hiki kiliasisiwa na Rais wa awamu ya tano Dk. John Magufuli kwa kuwapatia eneo hilo kubwa la ekari 10 bure, hata kijiti alivyokipokea Rais Dk. Samia ameendelea kuwapa ushirikiano kwa kuwapa miundombinu kama umeme na miundombinu ya barabara,” alisema.
Kwa upande wake, Mkuu wa Wilaya ya Bagamoyo, Shaibu Ndemanga alisema wamejiandaa kuwapokea wawekezaji kuhakikisha kila kinachozalisha kinapatikana kwa wakati.
“Sisi wilaya ya Bagamoyo tumejipanga vizuri kuhakikisha wawekezaji wetu wanawekeza na wenye nia ya kuwekeza tunawapokea na kuhakikisha kila kinachohitajika kinapatikana waweze kuwekeza.
“Kwa waliowekeza tunahakikisha tunawalinda, kuwasaidia kuendelea na uwekezaji wao, wawekezaji wengine waje Bagamoyo tumejipaga kuwapokea na shughuli zao zitakwenda vizuri,”.
Mkurugenzi wa uhusiano, Bakhresa Group, Husein Sufian alisema wamejipanga kuhakikisha uwekezaji wa sukari unaimarika.
Alisema kwa sasa wapo awamu ya tatu ya uzalishaji amabo walianza mwaka 2022/2023 na wanazalisha kulingana na miwa iliyopo ambapo kwa sasa uzalishaji umefikia tani 35,000.
“Mipango tuliyonayo ni kuendeleza mashamba ili awamu ya pili wafikie tani 60,000 na ikifika awamu tatu iwe tani 100,000 huko mbeleni tufikie uzalishaji wa sukari ya viwandani,” alisema.
Katibu wa Wizara ya Viwanda na Biashara, Dk. Hashil Abdallah alisema kamati imeona jinsi serikali ya Rais Dk. Samia inavyotafsiri kwa vitendo yanaliyobainisha katika miongozo mbalimbali ikiwemo Ilani ya Chama Cha Mapinduzi.
Alisema dhamira ya Rais Dk. Samia ni kuendeleza sekta ya viwanda nchini ambapo muwekezaji ameridhika na sera iliyopo na kukiri hakuna changamoto isiyotekelezwa na serikali.
“Walikuwa na changamoto ya barabara inatengenezwa, bwawa la maji Wizara ya Maji imefika kushirikiana na Wizara ya Kilimo hivyo kuna mkakati wa kujenga Bwawa kubwa la maji, walisema wanachangamoto ya gati Bagamoyo, serikali imethibitisha mwezi ujao mkataba wa ujenzi wake utakamilika,” alisema.
Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Viwanda,Biashara,Kilimo na Mifugo ikiongozwa na Makamu Mwenyekiti wake Mhe. Mariam Ditopile Mzuzuri ikiongozana na Mwenyeji wao Katibu Mkuu wa Wizara ya Viwanda na Biashara Dkt.Hashil Abdallah ikitembelea Kiwanda cha Sukari cha Bagamoyo kwa lengo la kukagua shughuli za sekta binafsi zinazosimamiwa na serikali ili kuhakikisha mwananchi anapata thamani ya kile anachostahiki.
Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Viwanda,Biashara,Kilimo na Mifugo ikiongozwa na Makamu Mwenyekiti wake Mhe. Mariam Ditopile Mzuzuri ikiwasili katika Ofisi za Kiwanda cha Sukari cha Bagamoyo wakipokelewa na Katibu Mkuu wa Wizara ya Viwanda na Biashara Dkt.Hashil Abdalah kwa lengo la kukagua shughuli za sekta binafsi zinazosimamiwa na serikali kuhakikisha mwananchi anapata thamani ya kile anachostahiki,Oktoba 08,2024 Wilaya ya Bagamoyo Mkoani Pwani.
No comments:
Post a Comment