Elimu : ECOBANK Tanzania yatoa Msaada katika Shule ya Sekondari ya Mugabe, Dar. - Wazalendo 25 Blog

Glory to Story.

PRINTING / GRAPHICS / DESIGN : 0784 643 633

Sunday, 20 October 2024

demo-image

Elimu : ECOBANK Tanzania yatoa Msaada katika Shule ya Sekondari ya Mugabe, Dar.


Ecobank Tanzania kwa kushirikiana na Taasisi ya Shule Direct wametoa msaada wametoa msaada wa kompyuta 10 (desktop), huduma ya mtandao, usajili kwa ‘Shule Direct’ kwa mwaka mmoja, madirisha ya Aluminium, Maabara, Madawati na Meza za Kompyuta kwa Shule ya Sekondari Mugabe iliyopo jijini Dar es Salaam ikiwa ni sehemu ya mkakati wa Kampuni ya Ecobank wa kutenga siku maalum kusaidia jamii katika maadhimisho ya uwajibikaji wa kijamii kwa kila mwaka ambayo huzishirikisha jamii zote ndani ya bara la Afrika.

Nchi zote 33 Barani Africa zenye benki ya Ecobank zimekuwa zikitenga siku maalumu kila mwaka (Ecobank Day) kusaidia jamani zinazoizunguka ili kutumiza lengo la kurudisha kwa Jamii.

Akizungumza wakati wa kutoa msaada wa Mkurugenzi Mkuu wa Ecobank Tanzania Bw. Charles Asiedu amesema benki hiyo inautaratibu wa kila mwaka wa kurudisha kwa jamii ambapo leo wameamua kutoa msaada wa vifaa hivyo ili kuongeza ufaulu katika shule hiyo ili kurahisisha wanafunzi kujifunza maarifa ya kisayansi na ujuzi wa vitendo kwa kubuni, kutengeneza na kutumia vifaa hivyo.

Amesema Ecobank Tanzania inadhamini mchango mkubwa wa shule ya Sekondari ya Mugabe kwa kuzalisha wataalam mbalimbali hapa nchini hivyo kutoa msaada huo itakuwa chachu kuweza kuinua kiwango cha ufahulu katika shule hiyo na pia dhana ya Benki kuwajengea Watoto na vijana hususani wa Kitanzania msingi sahihi wa maisha yao ya baadae.

Naye Mkuu wa shule Sekondari ya Mugabe Mathew Mchome ameishukuru Ecobank Tanzania kwa kuweza kutoa msaada katika shule hiyo kwani kufanya hivyo inawapa nguvu ya kuendelea kutoa Huduma kwa jamii.

PB3A3266
PB3A3264
Mkurugenzi Mkuu wa Ecobank Tanzania Bw. Charles Asiedu akizungumza wakati wa hafla ya kutoa msaada wa kompyuta 10 (desktop), huduma ya mtandao, usajili kwa ‘Shule Direct’ kwa mwaka mmoja, madirisha ya Aluminium, Maabara, Madawati na Meza za Kompyuta kwa Shule ya Sekondari Mugabe iliyopo jijini Dar es Salaam ikiwa ni sehemu ya mkakati wa Kampuni ya Ecobank wa kutenga siku maalum kusaidia jamii
PB3A3275
PB3A3286Mkuu wa shule Sekondari ya Mugabe Mathew Mchome akitoa neno la shukrani kwa uongozi wa benki ya Ecobank Tanzania ulioongozwa na Mkurugenzi Mkuu wa Ecobank Tanzania Bw. Charles Asiedu mara baada kupokea msaada wa kompyuta 10 (desktop), huduma ya mtandao, usajili kwa ‘Shule Direct’ kwa mwaka mmoja, madirisha ya Aluminium, Maabara, Madawati na Meza za Kompyuta kwa Shule ya Sekondari Mugabe iliyopo jijini Dar es Salaam ikiwa ni sehemu ya mkakati wa Kampuni ya Ecobank wa kutenga siku maalum kusaidia jamii
PB3A3384
Mkuu wa kitengo cha masoko na mawasiliano Ecobank Tanzania, Furaha Samalu akizungumza jambo katika hafla ya kutoa msaada katika Shule ya Sekondari Mugabe iliyopo jijini Dar es Salaam ikiwa ni sehemu ya mkakati wa Kampuni ya Ecobank wa kutenga siku maalum kusaidia jamii
PB3A3403
PB3A3409Mkurugenzi Mkuu wa Ecobank Tanzania Bw. Charles Asiedu (kushoto) akikabidi zawadi kwa baadhi ya wanafunzi ikiwa ni sehemu ya mkakati wa Kampuni ya Ecobank wa kutenga siku maalum kusaidia jamii ambapo Nchi zote 33 Barani Africa zenye benki ya Ecobank zimekuwa zikitenga siku maalumu kila mwaka (Ecobank Day) kusaidia jamani zinazoizunguka ili kutumiza lengo la kurudisha kwa Jamii.
PB3A3300

PB3A3322

PB3A3332

PB3A3353

PB3A3371

PB3A3378

PB3A3479
PB3A3484
Wafanyakazi wa Ecobank Tanzania wakiongozwa na Mkurugenzi Mkuu wa Ecobank Tanzania Bw. Charles Asiedu wakiwa kweye picha ya pamoja na Walimu wa Shule ya Sekondari ya Mugabe wakiongozwa na Mkuu wa shule hiyo Mathew Mchome pamoja na baadhi ya wanafunzi wa shule hiyo.

No comments:

Post a Comment

Contact Form

Name

Email *

Message *

Tuwasiliane

Name

Email *

Message *