Waziri Mkuu Mstaafu, Jaji Joseph Sinde Warioba akizungumza leo Septemba 19, 2024 wakati kongamano lililoandaliwa na Kituo cha Demokrasia Tanzania (TCD) ikiwa ni katika kuadhimisha siku ya Demokrasia duniani ambayo hufanyika kila mwaka ifikapo Septemba 15.
Mwenyekiti waKituo cha Demokrasia Tanzania(TCD), Freeman Mbowe akizungumza leo Septemba 19, 2024 wakati kongamano lililoandaliwa na Kituo cha Demokrasia Tanzania (TCD) ikiwa ni katika kuadhimisha siku ya Demokrasia duniani ambayo hufanyika kila mwaka ifikapo Septemba 15.
Mkurugenzi Mtendaji Kituo cha Demokrasia Tanzania(TCD) Bernadetha Kafuko akizungumza leo Septemba 19, 2024 wakati kongamano lililoandaliwa na Kituo cha Demokrasia Tanzania (TCD) ikiwa ni katika kuadhimisha siku ya Demokrasia duniani ambayo hufanyika kila mwaka ifikapo Septemba 15.
Na Avila Kakingo, Michuzi Tv
WAZIRI Mkuu Mstaafu, Jaji Joseph Sinde Warioba ametaja mambo matatu yanayoonesha kuwa Demokrasia nchini imeimarika licha ya kuwepo na dosari mbalimbali.
Akizungumza leo Septemba 19, 2024 wakati kongamano lililoandaliwa na Kituo cha Demokrasia Tanzania (TCD) ikiwa ni katika kuadhimisha siku ya Demokrasia duniani ambayo hufanyika kila mwaka ifikapo Septemba 15.
Katika kuadhimisha siku ya Demokrasia duniani TCD imewaleta pamoja wadau wa demokrasia wakiwemo taasisi za serikali, vyama vya kisiasa, viongozi wastaafu, wanadiplomasia wadau wa maendeleo, asasi za kirai, wanataaluma viongozi wa dini na wanahabari kwaajili ya kufanya mapitio na kupendekeza maboresho katika kuimarisha Demokrasia nchini.
Lengo kuu la Kongamani la maadhimisho hayo ni kupitisha ripoti ya kwanza ya tathmini ya mwaka ya TCD kuhusu hali ya demokrasia nchini, kujenga uelewa wa pamoja juu ya demokrasia shirikishi pamoja na kutoa nafasi kwa wadau kuandaa na kubadilishana mawazo.
Jaji Warioba ametaja mambo hayo kuwa ni kuangalia namna demokrasia inavyosaidia jamii katika kufanya mikusanyiko mbalimbali na kukusanya mawazo yao kwaajili ya kuleta maendeleo nchini.
Kwamba watu wawe huru kuamua mambo yao, kitendo hicho ni kitendo cha maendeleo.
"Kama Demokrasia ni watu, hii demokrasia tunayoizungumza kwa sasa wananchi wanaitazamaje, kuanzia kwenye vyama vya siasa, haki za wanasiasa, haki wa Wananchi je demokrasia hii imewasaidia." Amehoji
Amesema kuwa Katiba iliweka utaratibu ingawa sio watu wote wanaoshiriki katika uendeshaji wa nchi, katiba iliweka utaratibu huo ili kuwawezesha wachague wawakilishi wao na hiyo ndio demokrasia.
"Tujiulize tunapofanya kazi, Wananchi wanahaki ya kuchagua wawakilishi wao? Pia tunazungumza haki za vyama vya siasa, sio haki za wananchi na ukisikiliza wananchi wanamalalamiko yao ya demokrasia, kwamba katiba inawapa haki ya kuteua wawakilishi wao lakini haki hiyo inapokonywa na vyama vya siasa." Ameeleza Jaji Warioba
Pia amesema kuwa wananchi hawanahaki ya kuchagua wale wanaowataka vyama vya siasa ndivyo vinavyo amua nani awawakilishe wananchi.
Amesema kuwa wakati wa TANU na CCM, walijaribu kutafuta utaratibu ambao ungewaongoza kuteua watu ambao wanatakiwa na wananchi, lakini mgombea kwenye kura za maoni kunakuwa na kuwapendekeza watu wengine.
Akizungumzia jambo la pili Jaji Warioba amesema kuwa ni namna ya kuratibu mchakato wa uchaguzi, namna ya kupiga kura na namna ya kuhesabu kura mpaka kutangazwa matokeo ya uchaguzi uwe uwazi licha ya kuwepo dosari mablimbali zinazojitokeza lakini inatakiwa kufanyiwa tathmini na uvumbuzi wa dosari zinazojitokeza ili kuwe na utawala bora.
Pia amesema kuwa kwa sasa mambo yameanza kuchanganywa kati ya utawala bora na Demokrasia licha ya kuwa vitu hivyo haviko sawa.
Tatu ni kuwepo kwa Umoja na amani ya nchi iwepo. Jaji warioba amesema kuwa vyama vya siasa vimeanza kuingilia amani na umoja wetu ndio maana kwasasa kumeanza kujitokeza kutugawa kwa Ukabila, Udini, pia wanasiasa wameanza kutumia majukwaa ya dini kisiasa
"Licha ya kuwa Tanzania kunamakabila 128 lakini ukabila unanyemelea kutugawa, pia ubaguzi wa kuwa Mnzazibari na Mnzibara sasa umoja wetu unasambaratika." Amesema Jaji Warioba
Kwa Upande wa Mwenyekiti wa TCD, Freeman Mbowe amesema kuwa katika kipindi kifupi ambacho walishaanza kuona matunda ya demokrasia katika nchi kwamba kiwango kikubwa cha uhuru wa kufanya siasa ikiwamo kufanya mikutano ya hadhara, maandamano yalifanyika nchi nzima kwa amani na kwa ushirikiano mkubwa kati ya vyama vya siasa na vyombo vya ulinzi na usalama, kazi za siasa zikafanyika bila kuwa na tabu yoyote,
tukaanza kuamini tunajenga utaratibu ulio bora, unaolipeleka taifa letu katika chaguzi ambazo zitatupatia viongozi watokanao na mapenzi ya wananchi.
"Pamoja na hofu nyingi kutokana na kanuni na taratibu zetu zote za uchaguzi, angalau kwa nje palionekana pana utulivu na kazi za siasa zilifanyika lakini ghafla ule uimara tuliokuwa tunaupata katika taifa haujawa endelevu, tukaanza kuona kukamatwa kwa viongozi wetu (CHADEMA) na kupigwa na vyombo vya dola, na mpaka leo wahusika wapo na ikaonekana ni jambo la kawaida na ni haki ya makundi fulani kukabiliana na adhabu kama hizo wakati bado tunatafakari
kulikoni?" Amehoji Mbowe
Amesema kuwa kila kukicha kunakuwa na matukio yanayojeruhi roho za watu, watu wanajeruhiwa na kukamatwa.
Amesema kuwa anapata wakati mgumu kujadili ripoti ya Demokrasia ya mwaka mmoja licha ya kuwepo matukio hayo yote.
Pia amesema anatamani Taifa hili liongozwe kwa Katiba iliyo bora ambayo itazaa sheria iliyo bora na vyote kwa pamoja vitatengeneza ustawi ulio bora kwa raia wote, kwa muda mrefu katika nchini yetu kumekuwa na utamaduni wa waliopo katika madaraka kuamini utashi wa Kiongozi Mkuu ndio unapaswa kuwa dira ya taifa,haipaswi kuwa hivyo.
"Ili demokrasia iwe na maana lazima wakati wote itambue haki, lazima pawe na utashi wa kisiasa na utashi huu wa kisiasa utoke zaidi kwa wale waliopoewa dhamana ya kuongoza Taifa.
"Nimesema kwetu ni mwezi wa majonzi kwa sababu tunapoizungumza demokrasia na haki ya kuishi, haki kwa Watu wote, basi iwe kwetu sote, na sio katika kikundi fulani cha Watu wawe ni watu wa kulia, watu wa kuomboleza, nimesema Ndugu zangu huu kwetu ni mwezi mgumu kwasababu tumewapoteza wenzetu na tunaendelea kutokujua wenzetu wako wapi, Watumishi wenzetu katika wajibu wa siasa ambao katika mazingira ya kutatanisha wamepotea katika uso wa dunia." Ameeleza kwa hisia.
No comments:
Post a Comment