Biashara : Benki ya CRDB kushirikiana na wadau kimataifa Mpango wa MADE Alliance Africa kukuza ujumuishi wa Kidijitali kwa Wakulima nchini - Wazalendo 25 Blog

Glory to Story.

Habari Mpya

PRINTING / GRAPHICS / DESIGN : 0784 643 633


PRINTING / GRAPHICS / DESIGN : 0676 643 633

Thursday, 26 September 2024

Biashara : Benki ya CRDB kushirikiana na wadau kimataifa Mpango wa MADE Alliance Africa kukuza ujumuishi wa Kidijitali kwa Wakulima nchini


Benki ya CRDB inajivunia kutangaza ushirika katika mpango wa uwezeshaji na ujumuishi wa wakulima kidijitali nchini kupitia programu ya  'MADE Alliance: Africa'. Programu hiyo inatekelezwa kwa ushirikiano wa MasterCard, Benki ya Maendeleo Afrika (AfDB), pamoja na Serikali, ambapo Dola za Marekani bilioni 300 zinetengwa kusaidia ujumuishi wa kidijitali kwa wakulima barani Afrika. 

Kupitia mpango huo wa Tanzania ambao umezinduliwa kando ya Mkutano Mkuu wa Umoja wa Mataifa (UNGA 79), Benki ya CRDB inadhamiria kuongeza uwekezaji katika mifumo na huduma za kidijitali ili kuchochea ujumuishi wa kifedha kwa wakulima, pamoja na kuboresha uzalishaji kupitia uwezeshaji wa matumizi ya techolojia za kisasa za kilimo.

Katika hafla hiyo ya uzinduzi wa utekelezaji wa programu ya MADE Alliance Tanzania ambayo ilishuhudiwa na Waziri wa Uwekezaji na Mipango, Prof. Kitila Mkumbo pamoja, Balozi wa Tanzania nchini Marekani, Mhe. Elsie Kanza, na viongozi mbalimbali wa Serikali, Benki ya CRDB iliwakilishwa na Makamu Mwenyekiti wa Bodi ya Wakurugenzi wa Benki ya CRDB, Prof. Neema Mori, Mkurugenzi Mtendaji wa CRDB Bank Foundation, Tully Esther Mwambapa, Mkurugenzi Mtendaji wa CRDB Bank Burundi, Fred Siwale, Mkurugenzi wa Hazina, Alex Ngusaru, pamoja na viongozi wengine waandamizi wa benki.
Benki ya CRDB inaongoza katika uwezeshaji sekta ya kilimo ikitoa zaidi ya asilimia 60 ya mikopo yote katika sekta hii adhimu katika uchumi wa Taifa letu. Aidha, Benki inafanya uwezeshaji kwa wakulima kupitia huduma bunifu za bima ya afya kwa kushirikiana na NHIF, na bima za mazao kupitia kampuni yetu tanzu ya CRDB Insurance Company (CIC) Ltd.

Benki ya CRDB inajivunia pia kuwa Benki pekee iliyojikita katika kutoa elimu ya fedha na kuchcochea ujumuishi wa kidijitali kwa wakulima kote nchini kupitia programu ya IMBEJU Kilimo inayotekelezwa na kampuni yetu tanzu ya CRDB Bank Foundation, ambapo wanawake na vijana katika sekta ya kilimo wamekuwa pia wakipatiwa mafunzo ya matumizi sahihi ya teknolojia za kisasa katika kilimo ili kuongeza tija katika shughuli zao.

No comments:

Post a Comment