Naibu Waziri wa Fedha, Mhe. Hamad Chande (Mb.) ameagiza Bodi ya Wataalamu wa Ununuzi na Ugavi (PSPTB) ihakikishe watu wanaofanyakazi za Ununuzi na Ugavi wamesajiliwa na Bodi hiyo ili kukidhi matakwa ya Sheria ilioianzia PSPTB
Agizo hilo limetolewa na Mhe. Chande wakati wa ufunguzi wa mafunzo ya uwasilishwaji wa Malalamiko/ Rufaa za Ununuzi wa Umma katika Mfumo wa NeST yanayofanyika kwa siku mbili Jijini Dar es Salaam.
Waziri Chande ameielekeza PPAA kuhakikisha kuwa inashirikiana na PSPTB katika maamuzi mnayotoa ili PSPTB waweze kuwachukulia hatua stahiki wataalamu wa ununuzi na ugavi pindi wanaokiuka maadili ya taaluma yao.
Pia amewaasa maafisa ununuzi wa taasasi za Serikali kuhakikisha kuwa shughuli zote za ununuzi wa umma zinafanyika katika mfumo wa ununuzi wa umma kieletroniki (NeST) ikiwa ni pamoja na kutumia moduli ya kuwasilisha malalamiko kieletroniki.
Naibu Waziri wa Fedha, Mhe. Hamad Chande (Mb.) akizungumza wakati wa ufunguzi wa mafunzo ya uwasilishwaji wa Malalamiko/ Rufaa za Ununuzi wa Umma katika Mfumo wa NeST yanayofanyika kwa siku mbili Jijini Dar es Salaam.
Mkuu wa Kitengo cha Masoko na Uhusiano kwa Umma ( PSPTB), Shamim Mdee akizungumza jambo wakati wa ufunguzi wa mafunzo ya uwasilishwaji wa Malalamiko/ Rufaa za Ununuzi wa Umma katika Mfumo wa NeST yanayofanyika kwa siku mbili Jijini Dar es Salaam.
Naibu Waziri wa Fedha, Mhe. Hamad Chande (Mb.) akiwa kwenye picha ya pamoja na wafanyakazi wa Bodi ya Wataalamu wa Ununuzi na Ugavi (PSPTB) wakati wa ufunguzi wa mafunzo ya uwasilishwaji wa Malalamiko/ Rufaa za Ununuzi wa Umma katika Mfumo wa NeST yanayofanyika kwa siku mbili Jijini Dar es Salaam.
No comments:
Post a Comment