Teknolojia : Serikali yafanya Maboresho kwenye ada za usajili kwa Mitandao, Redio na Televisheni. - Wazalendo 25 Blog

Habari Mpya

Glory to Story.


Post Top Ad


26 Aug 2021

Teknolojia : Serikali yafanya Maboresho kwenye ada za usajili kwa Mitandao, Redio na Televisheni.


Naibu Katibu Mkuu wa Wizara ya Mawasiliano na Teknolojia ya Habari, Dkt  Jim Jonazi akizungumza wakati wa kuhitimisha mkutano wa kukusanya maoni kuhusu maboresho ya maudhui mitandaoni leo Agosti 26, 2021 jijini Dodoma.
Mkuu wa Kitengo cha Ufuatliaji  cha Mamlaka ya Mawasiliano Tanzania (TCRA), Dkt. Philip Filikunjombe  akifafanua jambo wakati wa mkutano wa kukusanya  maoni ya wadau kuhusu maboresho ya kanuni za maudhui mitandaoni jijini Dodoma leo Agosti 26,2021.
Mkurugenzi Msaidizi wa Idara ya Habari Maelezo, Patrick Kipangula akielezea kuhusu sheria  ya huduma ya vyombo vya habari inayowataka waandishi wa habari kuwa na   vyeti vya ngazi ya diploma kuanzia Januari  Mosi 2021.

Sehemu ya wadau wakiwa katika mkutano huo.
Mwandishi wa Habari na Wakili, James Marenga akitoa maoni kwenye mkutano huo na kushauri kupunguza faini kwa wanaofanya makosa .
Mwenyekiti wa Jukwaa la Wahariri Tanzania ambaye pia ni  mwanasheria, Deodatus Balile akitoa maoni ambapo alishauri kuongeza muda wa usajiri wa leseni za maudhui mitandaoni kutoka miaka mitatu hadi mitano na ada ya mwaka irekebishwe.
Meneja Miradi wa Kampuni ya Star Times,Abdulkadil Mbeo akichangia hoja maboresho hayo.
Dkt Vernon Fernandos kutoka Agape akichangia maboresho hayo.
Sehemu ya wadau wakiwa kwenye mkutano huo.






Mwenyekiti wa MOAT/ MUX, Samwel Nyalla akichangia wakati wa maboresho hayo.



Na Richard Mwaikenda, Dodoma


SERIKALI iko mbioni kupunguza ada za leseni za maudhui mtandaoni kutoka sh. 100, 000 ya usajili hadi sh. 50,000 na ada ya mwaka kutoka shilingi milioni moja hadi laki tano kwa mwaka.


Maboresho hayo yamewasilishwa na Mkuu wa Kitengo cha Ufuatiliaji  cha Mamlaka ya Mawasiliano Tanzania (TCRA), Dkt. Philip Filikunjombe katika mkutano wa kukusanya  maoni ya wadau kuhusu maboresho ya kanuni za maudhui mitandaoni jijini Dodoma leo Agosti 26,2021.


Dkt. Filikunjombe ametaja mambo mengine muhimu Katika Marekebisho ya Kanuni za Maudhui Mtandaoni, 2020 kuwa ni; Kutofautisha kati ya Utoaji wa Maudhui kama chombo cha habari na maudhui mengine, Kuondoa masharti kwa Internet Cafes, Kuainisha Aina za Leseni za Utoaji wa Maudhui Mtandaoni, Kuondoa hitaji la Leseni kwa ajili ya Simulcasting pamoja na Kuondoa zuio la Matangazo ya Kubahatisha (Online Betting, Gambling).


Ametaja kanuni zingine zinazofanyiwa marekebisho kuwa ni;Kanuni za Maudhui,Utangazaji - Redio na Televisheni, 2018, Kanuni za Miundombinu ya Utangazaji, 2018 na Kanuni za Leseni, 2018.


Mdau nakuomba uendelee kusoma maboresho mengine yafuatayo hapa chini:


Mambo Muhimu (Key Issues) Katika Marekebisho ya Kanuni za Maudhui (Utangazaji - Redio na Televisheni) 2018 ni;

Kuainisha Wigo wa Utoaji Huduma kwa Leseni za Utangazaji-Redio Leseni ya Kiwilaya (three AoP within one region), Kuruhusu Audio Visual Radio Broadcasting, Kuondoa hitaji la kuwa na leseni kwa ajili ya Hookup. 


Mambo Muhimu (Key Issues) Katika Marekebisho ya Kanuni za Miundombinu ya Utangazaji, 2018 ni;

Kuruhusu Matangazo ya Kibiashara katika Chaneli za Televisheni za Kulipia (yasizidi dkk 5 kwa saa),

Kuruhusu Urushaji wa Matukio Mubashara (live events) katika Chaneli za Televisheni za Kulipia,Kuruhusu Chaneli za Free to Air kuonekana katika ving’amuzi vyote ikiwa ni pamoja na vile vya channeli za kulipia (zionwe bila kulipia).


Mambo Muhimu (Key Issues) Katika Marekebisho ya Kanuni za Leseni (the Licensing Regulations), 2018 ni;

Kuondoa hitaji la leseni wa wauzaji wadogo wa Vifaa vya 

Mawasiliano vya kielektroniki (sellers of electronic  communication equipment), Kuainisha Aina Mpya ya Leseni maalum kwaajili ya Vituo vya Kuhifandhia taarifa (Public Data Centres), Kuanzisha leseni mpya ya Utangazaji “Special Content Televisheni/Radio”, Kubadili utozaji wa ada za leseni USD to Tshs (kwa leseni za Utangazaji), Kupunguza ada na tozo mbalimbali za leseni (nyongea za ya kwanza ya Kanuni),Community Content Provision-Kuwa leseni ndogo.


Kupunguza ada za leseni- Kwa mfano;

Ada za Kibali cha Mawasiliano kwa njia ya Redio (Cross border –Commercial VSAT from USD 3,000 to 60USD na USD50 kwa zile za private, Ada za Utangazaji redio 

(National-32M/20,000$), Regional – 24m fro 15,000$ na  District-3.2m/2,000$

c) Ada za Utangazaji Televisheni (National-32M/28,000$)na District-3.2m/4,000$.


HITIMISHO


Maboresho ya Kanuni ni suala muhimu ktk kuhakikisha utoaji wa huduma za mawasiliano unaendana na mabadiliko ya teknolojia na uhalisia wa mazingira yaliyopo;

Pamoja na maboresho haya, ni dhamira ya Serikali kuendelea kufanya maboresho ya Kanuni kila itakapohitajika;

Wadau mnaombwa kuendela kutoa ushirikiano ili kujenga 

Tanzania yenye hududuma bora za mawasiliano ambazo ni chachu ya maendeleo ya nchi yetu.

No comments:

Post a Comment

Post Top Ad