Teknolojia : Mkutano wa Kimataifa wa Nane wa Wiki ya Kijani - Wazalendo 25 Blog

Glory to Story.

Habari Mpya

PRINTING / GRAPHICS / DESIGN : 0784 643 633

Wednesday, 11 April 2018

Teknolojia : Mkutano wa Kimataifa wa Nane wa Wiki ya Kijani



Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano Prof. Makame Mbarawa (Mb.) akihutubia kwenye Mkutano wa Nane wa Wiki ya Kijani, unaowakutanisha wadau mbalimbali wanao simamia na kutengeneza vifaa na miundombinu mbalimbali ya Tehama. Mkutano huo unatarajia kuangalia namna mbalimbali za kupambana na matumizi ya Tehama yanayochafua mazingira; umehudhuriwa na viongozi mbalimbali kutoka Serikalini ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na Serikali ya Mapinduzi Zanzibar, akiwemo Waziri wa Ujenzi, Usafirishaji na Mawasiliano Zanzibar Dkt. Sira Ubwa (Mb.), Katibu Mkuu (Mawasiliano) Wizara ya Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano Dkt. Maria Sasabo, Naibu Katibu Mkuu wa Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki Balozi Ramadhan Mwinyi, Mkurugenzi wa ITU (International Telecomunication Union), Dkt. Chaesub Lee, Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya Mawasiliano Tanzania, Mhandisi Kilaba. Mkutono huo unafanyika katika Hoteli ya Sea Clif Mangapwani, Zanzibar kuanzia tarehe 9-12, Aprili 2018.

Waziri wa Ujenzi, Usafirishaji na Mawasiliano Zanzibar, Dkt. Sira Ubwa, akiwakaribisha wajumbe wa mkutano huo visiwani Zanzibar na kuelezea faida ya mkutano kufanyikia Unguja. Alisema kwa mazingira ya sasa, changamoto iliyopo mbele yetu ni kushirikiana kwa pamoja ili kuziepusha nchi zetu na uharibifu utokanao na matumizi ya vifaa chakavu vya kielektroniki. Mhe. Dkt. Sira alitumia fursa hiyo kuwapongeza kwa mjadala muhimu utakaoendelea wa utunzaji wa mazingira na kuwasihi wasiache kutembelea vivutio vya asilia vilivyopo visiwani humo.

Mkurugenzi wa International Telecommunication Union (ITU) Dkt. Lee akizungumza kuhusu mjadala na maazimio ya mkutano huo muhimu wa kimataifa wakati wa ufunguzi wa Mkutano wa 8 wa Wiki ya Kijani.



(Juu na Chini) Sehemu ya wajumbe na washiriki mbalimbali wa mkutano huo wakifuatilia kwa makini hotuba za viongozi wakati wa ufunguzi wa mkutano.

Mkutano ukiendelea.
Waziri wa Ujenzi, Usafirishaji na Mawasiliano Zanzibar, Dkt. Sira Ubwa, akifurahia jambo na Naibu Katibu Mkuu Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki wakati wa vikao vya pembezoni wakati wa Mkutano wa Nane wa Wiki ya Kijani.

Balozi Mwinyi akielezea jambo huku Dkt. Ubwa na Dkt. Sasabo wakimsikiliza.

Picha ya pamoja mara baada ya kumalizika kwa ufunguzi wa Mkutano wa 8 wa Wiki ya Kijani, unaoendelea kwenye Hoteli ya Sea Cliff Zanzibar tarehe 9-12, Aprili, 2018.

No comments:

Post a Comment