Matukio : Waziri Mkuu, Majaliwa Kassim Majaliwa Aweka Jiwe la msingi la mradi wa Ujenzi, Dodoma - Wazalendo 25 Blog

Glory to Story.

Sunday, 22 April 2018

demo-image

Matukio : Waziri Mkuu, Majaliwa Kassim Majaliwa Aweka Jiwe la msingi la mradi wa Ujenzi, Dodoma



PMO_0065
Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akisalimiana na balozi wa Poland nchini, Mhe. Krzysztof Buzalski wakati alipowasili kwenye viwanja vya magahla ya Wakala wa Hifadhi yaTaifa ya Chakula chino (NFRA) kuweka jiwe la msingi la mradi wa ujenzi wa magahala na vihenge vya kisasa, eneo la Kizota mjini Dodoma Aprili 21, 2018. Wapili kushoto ni Waziri wa Kilimo, Dkt. Charles Tizeba , kushoto ni Naibu Waziri wa Kilimo, Dkt, Mary Mwanjelwa na kulia ni Mjumbe wa bodi ya kampuni ya Freerum ya Poland, Bw. Piotr Wielesik.
PMO_0105
Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akiteta na balozi wa Poland nchini, Mhe Krzysztof Buzalski wakati alipoweka jiwe la msingi la mradi wa ujenzi wa maghala na vihenge vya kisasa katika eneo la Kizota mjini Dodoma Aprili 21, 2018.
PMO_0117
PMO_0172
Baadhi ya wageni waalikwa wakiwemo wabunge na Wakuu wa Mikoa wakimsikiliza Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa wakati aliopozungumza kabla ya kuweka jiwe la msingi la mradi wa ujenzi wa magahala na vihenge vya kisasa kwenye eneo la Kizota mjini Dodoma Aprili 21, 2018.
PMO_0177
Spika wa Bunge, Mhe.Job Ndugai akizungumza Katika sherehe ya uwekaji jiwe la msingi la maghala na vihenge vya kisasa kwenye eneo la Kizota mjini Dodoma, Aprili 21, 2018. Mgeni rasmi alikuwa ni Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa.
PMO_0199
Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akizungumza wakati alipoweka jiwe la msingi la mradi wa ujenzi wa magahala na vihenge vya kisasa katika eneo la Kizota mjini Dodoma Aprili 21, 2018.
PMO_0259
Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akiwaongoza viongozi kuweka jiwe la msingi la mradi wa ujenzi wa maghala na vihenge vya kisasa kwenye eneo la Kizota mjini Dodoma Aprili 21, 2018. Kutoka kushoto ni Waziri wa Nchi, Ofisi ya Waziri Mkuu, Sera, Bunge, Kazi, Vijana, Ajira na Wenye Ulemavu, Jenista Mhagama, Spika wa Bunge, Job Ndugai, Mwenyekiti wa CCM wa Mkoa wa Dodoma, Godwin Mkanwa, Balozi wa Poland nchini, Mhe. Krzystof Buzalski na kulia Waziri wa Kilimo, Dkt. Charles Tizeba.
PMO_0283
Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akiwa katika picha ya pamoja na baadhi ya viongozi walioshiriki kwenye sherehe ya kuweka jiwe la msingi la mradi wa ujenzi wa maghala na vihenge vya kisasa kwenye eneo la Kizota mjini Dodoma, Aprili 21, 2018.
PMO_0317
Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akiagana na balozi wa Poland nchini, Mhe Krzysztof Buzalski baada ya kuweka jiwe la msingi la mradi wa ujenzi wa magahala na vihenge vya kisasa katika eneo la Kizota mjini Dodoma Aprili 21, 2018. Watatu kulia ni Waziri wa Kilimo, Dkt. Charles Tizeba , kushoto ni Naibu Waziri wa Kilimo, Dkt, Mary Mwanjelwa na wapili kulia ni Mkuu wa Mkoa wa Dodoma, Bilinith Mahenge.(Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu)

No comments:

Post a Comment

Tuwasiliane

Name

Email *

Message *

Contact Form

Name

Email *

Message *