Wanariadha wakichuana vikali mbio za Nyika, Viwanja vya Magereza ,Kisongo Jijini Arusha. Picha na Gadiola Emanuel.
Na Yasinta Amos, Arusha
MKOA wa Arusha umeendelea na maandalizi yake katika mashindano ya mbio za nyika kusaka wanariadha watakaounda timu ya mkoa itakayochuana kitaifa hapo Mwakani.
Ikiwa ni Mara ya pili sasa zoezi la kusaka wanariadha hao likifanyika katika viwanja vya Magereza ambapo wanariadha kutoka vilabu mbalimbali wameonekana kuchuana vikali .
Mshindi kwa upande wa wanaume Josephat Joshua alishinda kwa muda wa wa 29:13:84 akifuatiwa na Silvester Simon Naali muda wa 29:21:70 wote kutoka timu ya klabu ya Polisi na nafasi ya tatu kumwendea mwanariadha Francis Damiani kutoka mbulu aliyemaliza kwa muda wa 29:30.
Kwa upande wa wanawake Noela Remy alimaliza kwa muda wa 22:14:32 akifuatiwa na Neema Paulo muda wa 22:58:19 wote kutoka klabu ya Talent .
Denisi Malle afisa habari kutoka kamati ya mbio za nyika Arusha alisema katika mbio hizo kwa mara ya kwanza wameweka mbio za watoto ili kuongeza hamasa na ushindani na kuibua vipaji kuanzia ngazi ya chini.
"Ushindani unaongezeka licha kuwa bado hamasa kwa wanawake inahitajika ili ushiriki wao uweze kuongezeka katika mbio zijazo," alisema.
Katibu mkuu wa Shirikisho la Riadha Tanzania (RT) Wilhelm Gidabuday aliwapongeza waandaaji kwa kuendelea kusimamia mbio hizo pia kushirikiana mbio za watoto kwa Mara ya kwanza kwani ni jambo ambalo likiwa endelevu litasaidia kuinua vipaji vya vijana wadogo.
"Bado nasisitiza kwa mikoa mingine nayo ijaribu kuoga utaratibu huu wa Arusha katika kusaka wanariadha bora watakaounda timu ya mkoa kwa ajili ya mashindano ya taifa,na napongeza Uongozi wa Riadha mkoa kwa juhudi katika kusaka wadhamini ambao ni Posso International 'USA' na Sunrise Radio kwa kuwaunga mkono," alisema Gidabuday.
Naye Mwenyekiti wa kamati ya mbio za nyika Rogart John Stephen aliwasihi wanariadha wote wajiuokeze kushiriki kwani ndio yatakayowaweka katika nafasi bora kwani wataendelea kuhamaisisha mchezo huu na jamii iruhusu watoto wao kushiriki Riadha.
"Tunashukuru wadhamini wote wanaojitokeza katika kuisaidia maendeleo ya mchezo huu na tunawaomba na wengine wajitokeze kuisaidia mchezo huu upige hatua zaidi," alisema Rogart
No comments:
Post a Comment