Utalii : Naibu Waziri, Japhet Hasunga atoa Tuzo kwa Waongoza Watalii Bora kwa Mwaka 2017 - Wazalendo 25 Blog

Glory to Story.

Habari Mpya

PRINTING / GRAPHICS / DESIGN : 0784 643 633

Monday, 16 October 2017

Utalii : Naibu Waziri, Japhet Hasunga atoa Tuzo kwa Waongoza Watalii Bora kwa Mwaka 2017



Naibu Waziri wa Maliasili na Utalii, Japhet Hasunga akizungumza katika hafla ya Waongoza watalii bora kwa mwaka 2017 iliyofanyika jana katika ukumbi wa Kimataifa wa Julius Nyerere jijini Dar es Salaam. Wengine ni waandaji wa tuzo hiyo. ( Picha na Lusungu Helela- Maliasili)

Naibu Waziri wa Maliasili na Utalii, Japhet Hasunga (katikati) akiwa na Naibu Katibu Mkuu wa Wizara ya Maliasili na Utalii, Dkt. Aloyce Nzuki ( wa nane kulia) wakiwa kwenye picha ya pamoja na Waongoza watalii bora kwa mwaka 2017 katika hafla iliyofanyika jana katika ukumbi wa Kimataifa wa Julius Nyerere jijini Dar es Salaam. Wengine ni waandaji wa tuzo hiyo. ( Picha na Lusungu Helela- Maliasili)

Naibu Waziri wa Maliasili na Utalii, Japhet Hasunga ( wa tano kushoto) akiwa Wakurugenzi wa taasisi zilizo chini ya Wizara ya Maliasili na utalii katika hafla ya Waongoza watalii bora kwa mwaka 2017 iliyofanyika jana katika ukumbi wa Kimataifa wa Julius Nyerere jijini Dar es Salaam. ( Picha na Lusungu Helela- Maliasili)

Mtendaji Bodi ya Utalii, Devota Mdachi akiwa na mshindi wa kwanza Peter Philemon aliyeibuka katika kipengele cha Wapagazi bora kwa mwaka 2017 mara baada ya kumkabidhi tuzo. Kushoto ni Katibu wa tuzo hiyo, Ally Mtemvu. Lengo la utoaji tuzo ni kuongeza morali na kuhamasisha utoaji wa huduma bora na wenye kuzingatia weledi wa hali ya juu kwa watalii nchini.

Mkurugenzi wa Idara ya Utalii Deogratius Mdamu akimkabidhi cheti na mshindi wa kwanza, Yohana Tumaini aliyeibuka katika kipengele cha Wapishi bora kwa mwaka 2017 ikiwa lengo la utoaji tuzo ni kuongeza morali na kuhamasisha utoaji wa huduma bora na wenye kuzingatia weledi wa hali ya juu kwa watalii nchini

Baadhi ya Waongoza watalii bora wakifuatilia kwa makini utoaji wa tuzo kwa mwaka 2017 katika hafla iliyofanyika jana katika ukumbi wa Kimataifa wa Julius Nyerere jijini Dar es Salaam. Picha na Lusungu Helela- Maliasili
Mkurugenzi wa Masoko wa Hifadhi ya Taifa ya Tanzania,Ibrahim Musa akikamkabidhi cheti mmoja wa washindi katika katika hafla ya utoaji tuzo kwa waongoza watalii iliyofanyika jana katika ukumbi wa Kimataifa wa Julius Nyerere jijini Dar es Salaam.

No comments:

Post a Comment