NA K-VIS BLOG/KHALFAN SAID, MADABA
WANANCHI wa Halmashauri ya mji wa Madaba, mkoani Ruvuma, wameipongeza serikali kwa kuwafikishia umeme kwenye eneo lao ambapo wamesema utabadilisha maisha yao.
Pongezi hizo zimetolewa Oktoba 11, 2017, kufuatia kukamilika kwa kazi ya kujenga njia ya kusafirisha umeme kwenye eneo hilo ikiwa ni pamoja na kuweka mtandao wa nyaya (wiring), kwenye eneo hilo na kwenye nyumba za wananchi kazi iliyokwenda sambamba na ufungaji wa transofoma pozo.
Kwa sasa Serikali kupitia Shirika lake la Umeme, TANESCO inatekeleza mradi mkubwa wa umeme wa Makambako-Songea ambao unahusisha ujenzi wa njia ya kusafirisha umeme wa msongo wa kilovolti 220Kv Transmision Lines na usambazaji umeme vijijini (Rural electrification), katika vijiji vya mkoa wa Njombe na Ruvuma ikiwa ni pamoja na kujenga vituo viwili vipya vya kupoza umeme, huko Madaba na Songea na upanuzi wa kituo kingine mjini Makambako.
“Nimefurahi sana eneo letu kupata umeme, kwa muda mrefu sana tumekuwa tukitegemea umeme wa solar, sasa nina matumaini makubwa nimeona kazi zinavyoendelea hapa za kuweka nguzo za umeme, kutandaza nyaya majumbani na kuweka transofa, na tumeambiwa tukae mkao wa kula kwani umeem utawaka muda wowote kuanzia hivi sasa.” Anasema Rehema Maluwa, (pichani juu).
Bi Maluwa, amesema, yeye ni mjasiriamali kwa hivyo ujio wa umeme utamuwezesha walau kutengeneza askrimu, na hivyo anatatarajia kujiongezea kipato kwa njia hiyo.Mwananchi mwingine Bw. Eliudi Msigwa, yeye anategeema umeme huo sio tu utawaharakishia maendeleo, pia utainua hadhi ya mji wao ambao kwa muda mrefu umekuwa hauna umeme.
Akizungumzia hatua iliyofikia hadi sasa katika kuhakikisha umeme unawaka kwenye Halmashauri hiyo, Meneja wa Mradi wa umeme wa Makambako-Songea, Mhandisi Didas Lyamuya, amesema, kilichobaki kwa sasa ni kuunganisha umeme majumbani.
Mwananchi mwingine Bi.Theresia Justin yeye amefurahishwa na taarifa za ujio wa umeme kwenye Hamlamshauri yao kwani tangu wapate uhuru hawajawahi kuwa na umeme, zaidi ya watu wenye uwezo kutumia majenereta na wengine umeme wa Solar.
“Niwahakikishie wananchi mwishoni mwa Novemba au mwanzoni mwa Desemba mwaka huu wa 2017, umeme utawaka kwenye Halmashauri ya Mji wa Madaba na wananchi watasherehekea Krismas wakiwa na umeme, alisema.
Kwa upande mwingine, kazi ya kujenga minara ya njia ya kusafirisha umeme, inaendelea kwa kasi ambapo hadi hivi sasa jumla ya minara, (nguzo kubwa) 266 imejengwa kati ya nguzo 710 ambazo zinatarajiwa kujengwa chini ya mradi huo.
Kwa upande wake Meneja wa TANESCO mkoani Ruvuma, Mhandisi Patrick Lwesya, amewataka wawekezaji kujenga viwanda vidogo, vya kati na vikubwa kwani upatikanaji wa umeme kwenye mkoa wake utakuwa wa uhakika na wa kutosha kutokana na utekeelzaji wa mradi huu unavyokwenda kwa kasi.
"Mradi huu ifikapo Septemba mwakani kwa asilimia 100 utakuwa umekamilika kwa hivyo wananchi wa Halmashauri ya Madaba, Songea, Mbinga na Namtumbo watakuwa na huduma ya umeme wa uhakika na wa kutosha na hivyo niwaombe tu kujiandaa kwa kuanzisha miradi midogo na mikubwa ya viwanda ili kuongeza pato lao na la taifa kwa ujumla." Alsiema Mhandisi Lwesya.
Wahandisi wa Shirika la umeem nchini TANESCO na mkandarasi kutoka kampuni ya m/s Isolux, wakijadiliana jambo pembezoni mwa moja ya transofa mpya zilizofungwa kwenye mji wa Madaba Oktoba 11, 2017.
Meneja wa TANESCO mkoa wa Ruvuma, Mhandisi Patrick Lwesya, akizungumza na wahariri kwenye eneo la ujenzi wa kituo kipya cha kupoza na kusambaza umeme wa kilovolti 220kV/33kV, eneo la Madaba.
Nyumba zikiwa na madishi ya tv kwenye Halmashauri ya mji wa Madaba mkoani Ruvuma ambazo bila shaka kwa muda mrefu wamekuwa wakitumia fedha nyingi kutokana na matumizi ya jenereta kupata umeme lakini ujio wa umeme wa TANESCO utapunguza gharama za uendeshaji.
Maendeleo ya ujenzi wa msingi wa kufungia mashine kituo cha Madaba, ukiendelea Oktoba 11, 2017.
Maendeleo ya ujenzi wa msingi wa kufungia mashine kituo cha Madaba, ukiendelea Oktoba 11, 2017.
Mafundi wa TANESCO kwa kushirikiana na mkandarasi kutoka kampuni ya India ya Kalpataru, wakiwa kwenye eneo la ujenzi wa minara ya kupitisha laini za umeme wa 220kV huko Iboya, Njombe.
Mafundi wa TANESCO kwa kushirikiana na mkandarasi kutoka kampuni ya India ya Kalpataru, wakiwa kwenye eneo la ujenzi wa minara ya kupitisha laini za umeme wa 220kV huko Iboya, Njombe.
Mafundi wa TANESCO kwa kushirikiana na mkandarasi kutoka kampuni ya India ya Kalpataru, wakiwa kwenye eneo la ujenzi wa minara ya kupitisha laini za umeme wa 220kV huko Iboya, Njombe.
Mhandisi kutoka kampuni ya Kalpataru, (kulia), akifafanua jambo kwa wahariri kwenye eneo la ujenzi wa minara ya kupitisha nyaya za umeme wa 220kV eneo la Iboya.
Wajariri wakiwa kazini eneo la ujenzi wa kituo kipya cha Madaba.
Mhandisi kutoka kampuni ya Kalpataru, (kulia), akiwatembeza wahariri kwenye eneo la ujenzi wa minara huko Iboya.
Kaimu Meneja Uhusiano wa TANESCO, Bi, Leila Muhaji, (kulia), na baadhi ya wahariri wakitembelea eneo la ujenzi wa minara huko Iboya.
Meneja Mradi wa Makambako-Songea, Mhandisi Didas Lyamuya, akifafanua jambo kwa waharri kwenye eneo al ujenzi wa kituo cha kupoza umeme Madaba mkoani Ruvuma Oktoba 11, 2017.
Mradi wa Makambako-Songea, umehamasisha ujenzi wa viwanda na ujenzi wa kiwanda cha kuchakata chai kinachomilikiwa na kampuni ya Uniliver huko Njombe.
Tayari eneo la ujenzi wa kiwanda hicho limefikishiwa umeme na TANESCO kama ambavyo transfoma pozo mpya iliyofungwa na Shirika hilo inavyoonekana jirani na eneo la ujenzi.
Meneja Mradi wa Makambako-Songea, Mhandisi Didas Lyamuya, akifafanua jambo kwa waharri kwenye eneo al ujenzi wa kituo cha kupoza umeme Madaba mkoani Ruvuma Oktoba 11, 2017.
No comments:
Post a Comment