Matukio : Timu ya Yanga yaifunga Kagera Sugar 2 -1 - Wazalendo 25 Blog

Habari Mpya

Glory to Story.


Post Top Ad


15 Oct 2017

Matukio : Timu ya Yanga yaifunga Kagera Sugar 2 -1


Kikosi kilichoanza cha Timu ya Kagera Sugar leo dhidi ya Timu ya Yanga SC ya Jijini Dar es salaam kwenye mchezo wa Ligi Kuu ya Vodacom Tanzania. Mchezo huu umepigwa kwenye Uwanja wa Kaitaba Mjini Bukoba. Picha na Faustine Ruta, Bukoba.
Kikosi cha Timu ya Yanga SC kilichoanza.

Timu zote mbili zikisalimiana kabla ya mchezo kuanza

Mgeni rasmi nae alipata muda akasalimia Timu zote mbili.

Timu ya Yanga Sc leo hii kwenye Uwanja wa Kaitaba wameibuka na ushindi wa mabao 2-1 dhidi ya wenyeji Kagera Sugar katika mchezo wa Ligi Kuu ya Vodacom Tanzania. Ushindi huo, unaifanya Yanga ifikishe pointi 12 baada ya kucheza mechi sita, Hadi mapumziko Yanga mdio walikuwa mbele kwa bao 1-0 dhidi ya Timu ya Kagera Sugar.


Bao hilo lilifungwa na Obrey Chirwa dakika ya 38 baada ya kumzidi ujanja beki wa Kagera Sugar Juma Nyosso na kumfunga kipa Juma Kaseja. Kipindi cha Yanga pili Yanga walifanikiwa kufunga tena bao lingine dakika ya 47 bao lililofungwa na Hajib baada ya kupewa pasi nzuri na Chirwa.
Dakika ya 52 Jaffar Kibaya alimfunga kipa wa Yanga kwa aliunganisha krosi kwa kichwa krosi iliyopigwa na Venence Ludovic. Mchezo huu umewapandisha Yanga kileleni kwa alama 12 huku Timu ya Kagera Sugar ikizidi kudidimia kwenye eneo hatari la mkiani.
Mchezaji beki wa Timu ya Kagera Sugar Juma Nyosso akikwaana na Chirwa kugombea mpira wa kichwa.

Chirwa tena na Beki wa Kagera Sugar Juma Nyosso.


Obrey Chirwa akishangilia bao lake dakika ya 38 kipindi cha kwanza

Chirwa mbele akishangilia bao lake kipindi cha kwanza baada ya kuifanikishia bao la kuongoza Timu yake ya Yanga. Picha na Faustine Ruta, Bukoba.


Gadiel Michael akimpongeza Chirwa

Shangwe kwa Wanayanga!

Chirwa akipongezwa na benchi la ufundi na kupewa mbinu zaidi za kuongeza bao. Yanga imeshinda bao 2-1 dhidi ya Timu ya Kagera Sugar. Picha na Faustine Ruta, Bukoba.





Shangwe kwa Yanga baada ya kufunga bao la pili kupitia kwa Hajib dakika 47.








Juma K Juma mlinda lango la Kagera Sugar akiwa hoi baada ya mchezo kumalizika kwa bao 2-1 dhidi ya Timu Kongwe ya Yanga SC kwenye Uwanja wa Kaitaba.

Faustine Ruta wa www.bukobasports.com(kulia) akiwa sambamba na blogger mwenzake MC Baraka wa Bukobawadau blog kwenye Uwanja wa Kaitaba Mjini Bukoba leo wakati wa Mapumziko.
Kikosi cha Kagera Sugar kilikuwa: Juma Kaseja, Mwaita Gereza, Adeyoum Ahmed, Juma Shemvuni, Juma Nyosso, Ally Iddi, Venence Ludovic, Ozuka Okochukwu, Jaffar Kibaya, Omar Daga na Christopher Edward/Themi Felix dk 64.
Kikosi cha Timu ya Yanga SC: Youthe Rostand, Juma Abdul, Gardiel Michael, Andrew Vincent, Kelvin Yondani, Said Juma Makapu/Raphael Daudi dk57, Pius Buswita, Papy Tshishimbi, Obrey Chirwa/Obrey Chirwa dk93, Ibrahim Hajib na Geoffrey Mwashiuya/Emmanuel Martin dk62.


Mashabiki waliingia kwa wingi Kaitaba leo



Mashabiki wa Timu ya Yanga walilizunguka Basi la Timu hiyo mara baada ya Mchezo kumalizika kwa Yanga SC kushinda bao 2-1 dhidi ya wenyeji Kagera Sagar.
Mashabiki wa Timu ya Yanga wakiwa wazunguka basi la Timu ya Yanga mara baada ya mchezo kumalizika nje ya Uwanja. Picha na Faustine Ruta, Bukoba
Mashabiki walitoka mapema Uwanjani, Huku wengi wakiteta juu ya Timu ya Kagera Sugar kuwa haina jipya kwa sasa. Baada ya kucheza michezo kadhaa na kupoteza huku ikiwa eneo baya la mkiani kwenye msimamo wa Ligi kuu Vodacom Tanzania Bara.

No comments:

Post a Comment

Post Top Ad